HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 08, 2020

SBL yazindua Bia mpya Kanda ya ZIwa

Na Mwandishi Wetu


KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL), imezindua bia mpya ya Pilsner Lager yenye ujazo wa mililita 300, mahususi kwa ajili ya wateja wake wa eneo la Kanda ya Ziwa.

Mkuu wa Kitengo cha Bia wa SBL, Anitha Msangi, alisema kuwa bia hiyo inazalishwa kwa kuwalenga wanaume hodari na shupavu.

Bia hii maarafu kwa msemo wake wa ‘Bia Imara kama Simba’ sasa itakuwa ikipatikana katika eneo lote ka Kanda ya Ziwa kwa bei nafuu ya Sh. 1,000 na hivyo kumwezesha kila mtu kufurahia ladha yake ya kipekee.

“Wakazi wa eneo la Kanda ya Ziwa wanafahamika kwa sifa yao ya uchapa kazi.
Pilsner Lager mililita 300 ambayo ni mahususi kwa ajili yao, sasa inapatikana katika eneo lote la kanda yao kwa ajili ya kuwaburudisha wakazi wa eneo hilo baada ya kazi za kila siku,” alisema Anitha.

Uzalishaji wa Pilsner unachagizwa na mfumo halisi wa utengenezaji wa bia hiyo maarufu duniani ambayo kwa mara ya kwanza ilitengenezwa huko Ulaya Mashariki.

Kwa miaka mingi, wapishi wa bia wa Afrika Mashariki wameendelea kudumisha namna ya utengenezaji wake unaohusisha uchujaji wa kipekee unaoipa bia hiyo ladha ya kipekee.

Kampuni ya SBL pia ndiyo mzalishaji wa bia yenye kimea kwa asilimia 100, Serengeti Premium Lager pamoja na bia laini maarufu yenye chimbuko lake hapa nchini Serengeti Lite.

SBL pia ni wasambazaji wa pombe kali zenye hadhi ya kimataifa kama vile Johhnie Walker, Ciroc, Smirnoff  Vodka, White Horse J&B na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment

Pages