HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 27, 2020

TAASISI YA BABA WATOTO YAKABIDHI VIFAA VYA KUJINGIKA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA

Wafanyakazi wa Taasisi ya Baba Watoto iliyoko Manzese jijini Dar es Salaam wakikabidhi vidhibiti maambukizi ya virusi vya corona kwa waendesha bodaboda na bajaji wa manispaa za Kinondoni na Ubungo. 



Na Mwandishi Wetu

TAASISI ya Sanaa ya Baba Watoto  kwa kushirikiana na madereva bodaboda, bajaji na mama lishe wa Manispaa za Kinondoni na Ubungo ambako watatoa elimu katika Kata 20 kupitia mradi COVID-19 Nitavuka.

Mradi huo ulioanza jana na kumalizika leo ambao malengo yake ni kuwafikia wadau zaidi ya 1500 watakaopata elimu sahihi ya kujikinga na janga la virusi vya corona.

Akizungumza jana katika hafla ya kugawa vifaa vya kujikinga na corona, mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Kinondoni, Abdullah Hemed alisema jamii inatakiwa kuendelea na taratibu za kuzingatia ushauri wa wataalam kwani pamoja na janga kupungua kwa kiasi kikubwa isiwe sababu ya kuacha kufuata masharti.

Hemed aliipongeza taasisi ya Baba Watoto kwa kuelekeza elimu ya janga la virusi vya corona katika maeneo ambayo yanahitaji elimu zaidi kwa sababu ya mikusanyiko mikubwa ya watu.

"Corona imekwisha kwa kiasi kikubwa, jamii isizembee kupiga vita, tukizembea utarudi kwa mara nyingine," alisema Hemed.

Naye Mkurugenzi wa Program wa Baba Watoto, Alfayo Wangwe alisema jamii inatakiwa kuendelea kujikinga na ugonjwa huo kwani haujakwisha kabisa.

"Tunamshukuru Rais John Magufuli kwa miongozo hadi kupungua kwa ugonjwa wa COVID-19, tunaiomba jamii iendelee kuzingatia ushauri wa wataalam," alisema Wangwe.

Baada ya hafla hiyo iliyofanyika katika  ofisi ya Baba Watoto, Manzese jijini Dar es Salaam, uongozi wa taasisi hiyo uligawa vifaa mbalimbali vyenye ujumbe wa kupiga vita virusi vya corona sambamba na wimbo maalum wenye ujumbe wa corona.

Awali elimu ya janga la virusi vya corona inatolewa kwenye Kata 20 ambazoni pamoja na Mwananyamala, Bunju, Tandale, Ndugumbi, Kunduchi, Kigogo, Makumbusho, Kawe, Kijitonyama na Hananasif (Kinondoni) huku kwa upande wa Ubungo ni pamoja na Manzese, Mabibo, Ubungo, Mbezi, Goba, Saranga, Kibamba, Makurumla, Makuburi na Msigani.

Mradi huo wa elimu ya kudhibiti virusi vya corona umefadhiliwa na taasisi ya Foundation for Civil Society ambao umegharimu shilingi milioni 35.

No comments:

Post a Comment

Pages