Mkuu wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Rukwa Hamza Mwenda amekabidhiwa ripoti ya
Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) nchini na Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo (pichani), ili kuyashughulikia yaliyomo ndani ya
ripoti hiyo na kuwakama wote waliohusika na ubadhirifu wa Chama Kikuu cha
Ushirika Mkoani humo.
Wangabo amesema
kuwa ripoti hiyo imetokana na uchunguzi uliofanya na COASCO mapema mwaka huu
ili kubaini ubadhirifu uliofanywa na uongozi wa chama hicho cha Ufipa Co-operative
Union (UCU) baada ya viongozi hao kuingia mkataba na kampuni ya pembejeo ya Eli
Agrovent Co, ili kununua mbolea jambo katika mchakato wa manunuzi ya mbolea
hiyo kiasi cha Shilingi milioni 277 zilipotea.
“COASCO walifanya
ukaguzi wa kina kuanzia mwezi Machi na wakatoa taarifa ndani ya Mwezi huo huo
mwaka huu 2020, na kubaini kwamba kuna mapungufu mengi yakiwemo ubadhirifu wa
hawa viongozi waliokaa ndani ya miezi sita tu, hawa viongozi wa chama cha
ushirika cha Ufipa (UCU), TAKUKURU nakukabidhi ripoti hii ya COASCO
Mkaishughulikie kwa kina, na wale wote waliohusika kufanya ubadhirifu
wakamatwe, warejeshe, fedha zirudishwe, nakukabidhi ripoti.”
“Hawa wote walioko
hapa wameteswa na viongozi wa vyama vya ushirika, na watesaji bado wapo, fedha
zimeokolewa kutoka kwa watu ambao hawakufuata sheria ya vyama vya ushirika na
kanuni zake, wakawatesa hawa kwahiyo waliowatesa wapo na wenyewe wapate mateso
yanayostahiki,” Alisisitiza.
Na kuongeza kuwa
wanachama wengi wamekuwa wakisita kujiunga na vyama hivi kutokana na ubadhirifu
unaofanywa na viongozi hao na hivyo kuogopa kujiunga na hivyo kumuagiza Mrajis
Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoani humo pamoja na maafisa ushirika katika
halmahsuri za mkoa huo kuhakikisha wanawapekuwa viongozi wote wabovu na kuwaondoa
kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.
No comments:
Post a Comment