Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (katikati) akikagua jana mmoja ya chumba cha darasa katika Shule ya Sekondari Usinge iliyojengwa kwa kutumia tofali zilizofyatuliwa na wanafunzi kupitia mfumo wa elimu ya Kujitegemea wa Kaliua (Kaliua EK Model). (Picha na Tiganya Vincent).
NA TIGANYA VINCENT
NA TIGANYA VINCENT
WAZAZI Mkoani Tabora wametakiwa kutenga siku moja katika
wiki ya kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya sekta ya elimu katika maeneo
yao kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya watoto kupata elimu.
Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Kaliua na Mkuu wa
Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya
shule iliyojengwa kutokana na nguvu za wanafunzi ambayo itasaidia kupunguza
uhaba wa vyumba vya madarasa.
Alisema muundo wa elimu ya kujitegemea unaotuumia
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa kushirikisha jamii na wanafunzi katika
ujenzi wa madarasa, maabara, mabweni na maktaba utasaidia kuboresha kiwango cha
elimu kwa wanafunzi kwa kuwa na mazingira rafiki ya upataji elimu.
Mwanri
aliipongeza Kaliua kwa uamuzi wake wa kutekeza wazo la Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa vitendo na kuagiza kuwa Mkoa
mzima ni lazima uanze kutumia wanaotumia Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua
wa ujenzi wa vyumba vya
madarasa na nyumba za walimu kwa kushirikisha wananfunzi na jamii ili kupunguza uhaba wa miundombinu hiyo.
Aidha alisema Elimu ya kujitegemea ni lazima itiliwe
mkazo ili iweze kuwaandaa wananfunzi kuwa tayari kujiegemea hata kama
hakuendelea na masomo ya juu.
Akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dkt. John Pima alisema kupitia mfumo wa
Elimu ya Kujiegemea ya Kaliua (Kaliua EK Model) wanafunzi wa shule za Msingi
waweze kufyatua tofali zaidi milioni 1.9
ambazo zimejenga vyumba vya madarasa 93, matundu ya vyoo 69 na nyumba za walimu
11.
Alisema kwa upande wa Shule za Sekondari wamefyatua na
kuchoma tofali zaidi ya laki 6 ambazo zimesaidia kujenga vyumba vya madarasa 56
na matundu ya vyoo 36.
Dkt. Pima aliongeza katika kuunga mkono juhudi za
wanafunzi na wananchi katika uekelezaji wa elimu ya kujitegemea ,Halmashauri
hiyo imetoa mabati bando 300 saruji mifuko
2,400 , mbao 2,072 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa katika
shule mbalimbali.
No comments:
Post a Comment