HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 26, 2020

MABALOZI 'WAMLILIA' RAIS MSTAAFU MZEE MKAPA

Baadhi ya mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, wamejitokeza kusaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa aliyeaga dunia Tarehe 24 Julai, 2020 jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Balozi Shinichi Goto akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa aliyeaga dunia Tarehe 24 Julai, 2020 jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Balozi, Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Misri chini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa nyumbani kwa Marehemu jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Finland chini Tanzania, Mhe. Riitta Swan akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa.
Balozi wa Oman hapa Nchini Mhe. Ally Abdallah Almahruqi akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Rais Mstaafu wa Tanzania Mzee Benjamin Mkapa nyumbani kwa marehemu jijini Dar es Salaam.
 Mwakilisi wa Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Adrian Fitzgerald akiwaelezea waandishi wa habari jinsi alivyomfahamu Rais Mstaafu Mzee Mkapa wakati alipokuwa nyumbani kwa marehemu jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages