HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 27, 2020

MFAUME KALANGUTI ASHINDA KURA ZA MAONI CCM KATA YA TANGINI

Na Victor Masangu, Pwani


KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani amewataka wanachama wa Chama hicho kuhakikisha wanachagua wagombea watakaowawakilisha vema katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwenzi Octoba mwaka huu.

 

Alisema ni vema kuzingatia kumpigia kura mgombea ambaye wanaamini atakwenda kuwa kielelezo kizuri kwa wananchi atakaposhindanishwa na wengine kutoka vyama vya upinzani.

 

Gama alitoa angalizo hilo  wakati wa mkutano wa kura za maoni katika kata ya Tangini Halmashauri ya mji wa Kibaha ambapo Mfaume Kalanguti aliongoza kura za maoni.

 

Katibu wa CCM kata ya Tangini Zuhura Sekelela alisema wamejipanga kata hiyo kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwezi Octoba.

 

" Tunataka Tangini sasa irejee kuongoza na CCM hatutaki kuwaachia wapinzqni tena, tunachotaka ni ushirikiano kwa wanachama tupate mwakilishi mzuri na atakayekubalika na wananchi. alisema Zuhura.

 

Alisema, ili kuendeleza mshikamano ni vema wanachama kujenga tabia ya kukubaliana na matokeo ya kura za maoni, na kuachana na tabia ya kwenda kwenye mikutano wakiwa na matokeo yao mfukoni changamoto ambayo imekuwa ikisababisha mgawanyo wa wanachama baada ya kura za maoni.

 

Akitangaza matokeo ya kura za maoni kata hiyo, Msimamizi wa uchaguzi Juma  Gama alimtaja Mfalme Kalanguti kuongoza kwa kupata kura 45, akifuatiwa na Philemon Mabuga aliyepata kura 28 na Alto Yombayomba kura 8.

 

Katika kata ya Mailimoja Ramadhani Lutambi aliongoza kura za maoni kwa kupata kura 75 akifuatiwa na Christopher Mjema kura 45 na Sudy Mohamed kura 8.

 

Kata ya Mkuza Focus Bundala kura 113, Erneus Mapunda kura 17, Ahmed Masimba kura 6, na katika kata ya Sofu Mussa Ndomba kura 33, Yusuph Mbonde kura 15 na Barton Mwaki kura 7.

 

Kata ya Nianjema Bagamoyo Abdul Pyalla alipata kura 56, Rajabu Swed 51 na Columbas Kayangwa kura 45.

No comments:

Post a Comment

Pages