Mhandisi wa Petroli wa MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Fabian Mwose, akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa (DITF). (Picha na Francis Dande).
Na Janeth Jovin
MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kupitia kaguzi zake
za mahesabu za wawekezaji za mwaka 2016-18 imefanikiwa kuokoa kiasi cha Sh. Bilioni 10.14 hivyo kupelekea kuongezeka kwa pato la serikali katika mgao wake wa uuzaji wa gesi asilia.
Pia PURA imesema kiasi cha gesi asilia kilichogundulika nchini katika maeneo ya nchi kavu na bandarini hadi kufikia Februari mwaka huu, takribani futi za ujazo Trilioni 57.54.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana katika maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa, Mhandisi wa Petroli wa Mamlaka hiyo, Fabian Mwose alisema mamlaka yao imekuwa na majukumu ya kuishauri Serikali juu ya masuala yanayohusu mkondo wa juu wa petroli katika utafutaji,uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini.
Alisema fedha hizo zimeokolewa siku za hivi karibuni kupitia kaguzi zake za mahesabu za mapato na matumizi za wawekezaji katika mkondo huo wa Petroli.
“Siku za hivi karibuni PURA kupitia kaguzi zetu za ndani tumeweza kuokoa fedha za serikali hizo kutoka kwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini katika mkondo wa juu wa petroli hii ni hatua kubwa kwetu katika kusimamia mkondo huo,”alisema
Aidha alisema kati ya futi za ujazo hizo zilizogundulika nchini ,gesi iliyogundulika nchi kavu ni futi za ujazo Trilion 10.41 huku kwa bahari Kuu ikiwa futi za ujazo Trilioni 47.13
“Kufikia mwezi februari 2020, uzalishaji wa gesi asilia kutoka visima vya Mnazi Bay ulikuwa wastani wa futi za ujazo Bilioni 2.6 kwa mwezi sawa na wastani wa futi za ujazo Milioni 87 kwa siku,”alisema na kuongeza
“Kwa upande wa uzalishaji wa gesi asilia kutoka visima vya Songo Songo ulikuwa wastani wa futi za ujazo Bilioni 2.14 kwa mwezi sawa na wastani wa futi za ujazo Milioni 71 kwa siku,”alisema
Alisema kutokana na takwimu hizo uzalishaji wa gesi asilia nchini kufikia wastani wa futi za ujazo Bilioni 4.75 kwa mwezi sawa na wastani wa futi za ujazo Milioni 158 kwa siku.
Mhandisi Mwose alisema PURA ni tofauti na Wizara ya Nishati, Mamlaka ya Kudhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) katika majukumu yake kwani yenyewe inafanya kazi ya kusimamia na kudhibiti mkondo wa juu wa petroli na mradi wa usindikaji wa gesi asilia kuwa kimiminika (LNG)
Alisema PURA inasimamia na kudhibiti LNG, tayari utekelezaji wa mradi huo umeanza mkoani Lindi na utakuwa na manufaa makubwa kwa nchi kwa kutoa kutoa zaidi ya ajira 40000 kwa vijana kupitia mradi huo.
“PURA katika kusimamia mradi wa LNG tutaweza kutoa ajira kwa watanzania wenzetu kwani mradi huo ni mkubwa na unagharimu zaidi ya Bilioni 30 za Kimarekani hivyo kupitia mradi huu utaweza kujenga uchumi katika nchi,”alisema

No comments:
Post a Comment