HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 05, 2020

PSPTB yatoa wimbo maalum wa uhamasishaji juu ya majukumu wanayoyafanya

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini Tanzania (PSPTB), Godfred Mbanyi (katikati), akipeana mkono na mfanyakazi wa bodi hiyo.


Na Janeth Jovin


BODI Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi nchini Tanzania (PSPTB), imezindua rasmi wimbo maalum wenye lengo la kuhamasisha shughuli mbalimbali zinazofanywa na bodi hiyo.

Akizindua wimbo huo jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Godfred Mbanyi amesema wimbo huo umejikita zaidi katika kuhamasisha juu ya majukumu ya Bodi ya PSPTB

Amesema wimbo huo pia umeweka msisitizo katika suala la usajili ambao kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha bodi hiyo wataalamu wote wa ununuzi na ugavi nchini wanatakiwa wawe wamesajiliwa na bodi ndipo waweze kufanya kazi za ununuzi.

Mbanyi amesema kwa mujibu wa kifungu cha 11cha sheria namba 23 ya mwaka 2007 iliyoanzisha bodi hiyo ni kosa kisheria kwa mtu yeyote kufanya kazi ya ununuzi na ugavi bila kusajiliwa na bodi.

"Wimbo huo utaweka msisitizo katika jambo hilo lakini pia utaelezea kazi mbalimbali za bodi kama kuwahimiza watu kuja kufanya mtihani ili waweze kuwa na sifa za juu za taaluma za ununuzi na ugavi," anasema

Aidha anasema katika wimbo huo umeweka kutangaza kazi za ushauri wanazozitoa na mafunzo mahususi ya taasisi za serikali na Binafsi .

"Katika wimbo huo tumeelezea mafanikio tuliyopata na kuonyesha taasisi ambazo wameweza kuzitolea mafunzo yaliyowasaidia kufanya vizuri katika eneo la manunuzi," anasema

Aidha Mbanyi ametoa wito kwa wataalamu waliopo vyuoni na makazini wajikite katika suala la usajili na wasisahau kupandishwa madaraja wasipofanya mitihani ya bodi ili waweze kupata sifa.

Wimbo huo utasambazwa katika vyombo vya habari,vyuo vyao na kwenye mikutano yao ili kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya kazi ya bodi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages