Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania, Macrice Mbodo, akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa.
Meneja Mkuu Rasilimali za Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba.
Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa Shirika la Posta Tanzania, Mwanaisha Said, akizungumza na waandishi wa habari juu ya walivyojipanga kuwahudumia wananchi wanatakaofika katika banda lao lililopo kwenye viwanja wa Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa.
NA JANETH JOVIN
SHIRIKA la Posta Tanzania limesema kuwa katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya mwaka huu limekuja na huduma mpya kwa wateja wake inayojulikana kwa jina la Posta Kiganjani ambayo itamuwezesha kila mtanzania kumiliki sanduku la barua kupitia simu yake ya mkononi.
Hayo yamebanishwa leo na Kaimu PostaMasta Mkuu wa shirika hilo, Macrice Mbodo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea banda la shirika hilo lililopo katika maonesho hayo ambayo maarufu kama sabasaba.
Mbodo anasema kwa sasa watanzania hawahitajiki tena kuwa na boski la barua na kwenda nalo katika ofisi za Posta kupata huduma bali atatakiwa kutumia simu yake ya mkononi ambayo ndio itakuwa sanduku lake la barua.
"Kwa maana nyingine kupitia huduma hii mpya, wananchi hawatasafiri tena kwenda katika jengo la Posta ili kuangalia barua zake ambazo wakati mwingine anakuta hazipo, lakini sasa iwe barua au vifurushi vikubwa na vidogo una uwezo kupitia simu yako ambayo umeosajili kupitia mfumo wa posta ikawa ndio sanduku lako ambalo litakupatia taarifa kila mahali.
Kama utakuwa umetumiwa mzigo au kifurushi chako kutoka hata Uingereza sisi tutakutumia meseji kwamba umefika na wewe sasa utachangua tukuletee nyumbani, ofisini au unakuja mwenyewe kuchukua," anasema Mbodo
Anasema wapo watanzania wengi wananunua mizigo kutoka nje ya nchi hivyo wakijiunga na huduma hiyo ya Posta Kiganjani maisha yatakuwa mepesi kwani watapata huduma kwa haraka na urahisi.
"Posta Kiganjani maana yake tunaitoa posta yote katika mfumo wa manyo na kuiingiza katika simu yako, anayetaka kujiunga na huduma hii anaingia website ya Posta ambayo ni www.posta.co.tz, ukiifungua utaona postakiganjani ambayo itakupa maelekezo mazuri kabisa namna ya kujiunga na kupata huduma," anasema
Hata hivyo anasema faidi ambayo watazipata kutokana na mfumo huo ni kuwapunguzia muda wananchi wa kutembea mahali walipo kwenda katika majengo ya posta kufatilia mizigo yao badala yake muda huo kuutumia kufanya majumuku mengine ya kujenga nchi na shirika kupata nafasi la kuwahudumia watu wengi kwa muda mfupi.
Aidha alisema huduma zingine ambazo shirika hilo inazitoa ni mfumo wa biashara mtandao ambao uwafanya watanzania kutangaza na kununua bidhaa zao ndani ya nchi na nje kupitia mtandao huo na wao kazi yao kuwapelekea bidhaa wateja hao mahali husika.
Hata hivyo anasema kwa sasa anatambua kuwa hakuna mtu anayemtumia mwenzake barua na hiyo imetoka na na ukuaji wa Teknolojia.
"Kwa sasa hakuna mtu na mtu ambaye wanaandikiana barua na kutumiana hiyo ni kwa sababu ya ukuaji wa teknolojia lakini barua za mtu na taasisi fulani bado zipo na haziwezi kuondoka, maana ili mtu aombe nafasi za kazi lazima aandike barua, hivyo watanzania watambue kuwa barua zilizopotea ni zile na mtu mmoja mmoja lakini za taasisi kwa taasisi bado zipo," alisema
Anasema kwa sasa shirika hilo limeamua kwenda kidigitali zaidi ili kuendana na kasi ya utekelezaji wa Sera mbalimbali za Serikali ya awamu ya tano.

No comments:
Post a Comment