Mwalimu wa kozi ya majokofu na viyoyozi kutoka Chuo cha VETA Pwani Haji Sinani akionesha meza aliyobuni inayoweza kupasha joto chakula na kufanya vinjwahi kuwa vya baridi.
Na Janeth Jovin
CHUO cha Ufundi stadi ch Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), Pwani kimebuni meza ambayo inauwezo wa kupasha joto chakula na kufanya vinywaji kuwa vya baridi.
Haji Sinani ni Mwalimu wa kozi ya majokofu na viyoyozi kutoka Chuo cha VETA Pwani ambaye ambebuni meza hiyo anasema inaweza kutumika katika maeneo ya migahawa pamoja hoteli.
Sinani anasema ameamua kubuni meza hiyo baada ya kuona aza wanayopitia watoa huduma ya chakula kulazimika kutumia ‘oven’ katika kupasha chakula kilicho ganda wakati mteja akiendelea kula.
Anasema meza hiyo itawarahisishia wafanyabiashara wa chakula kuweza kufanya mambo yao kwa ufanisi na kuvutia wateja wengi katika shughuli zao wanazofanya.
"Meza hiyo imefungwa injini ya jokofu chini na kutengenezewa mfumo wa baridi katika matundu maalumu ya kuweka chupa za vinywaji au glasi ili kuweza kuendelea kupoza vinywaji vyao"anasema Sinai nakuongeza kuwa
“Kila jokofu linapowaka huwa kuna joto linatoka ambalo linapotea bure sasa ili kuhakikisha na lenyewe linatumika vilivyo sehemu hiyo tumeweka maalumu kwa ajili ya kupasha chakula,” anasema Sinani
Anasema katika utengenezaji wa meza hizo huzingatia zaidi mahitaji ya wateja hivyo huweza kuwa na matundu manne ya kupozea vinywaji na sehemu moja ya kuchemshia chakula au kuongezwa idadi.
“Unaweza kuweka matundu nane ya kupozea vinywaji na matundu mawili ya kuchemshia chakula ni wewe tu kulingana na mahitaji yako na inatumia umeme kama kawaida,” anasema Sinani
Sinai anasema meza hizo huweza kutumia injini moya ya jokofu au ya zamani kulingana na mahitaji ya mteja huku meza hizo zikiwa tayari kwa ajili ya kuuzika.

No comments:
Post a Comment