Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Mbumbuli, akizungumza na waandishi wa habari leo katika banda la klabu hiyo lililopo katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Mwanachama wa Yanga, Esther Moshi akipanga mataji ya klabu hiyo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
Kiungo mkabaji na Nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi, akizungumza na waandishi wa habari katika banda la klabu hiyo lililopo katika Maonesho ya 44 ya Bishara ya Kimataifa (DITF).
Na Janeth Jovin
KLABU ya Yanga imewaita mashabiki wa timu hiyo kutembelea banda lao lililopo katika maonesho ya 44 ya biashara ya Kimataifa maarufu sabasaba ili kuweza kupata huduma mbalimbali ikiwamo ununuaji wa jezi na kuwasajili wanachama.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika viwanja vya maonesho hayo, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli anasema wanachama wanataofika katika banda hilo wanapata fursa ya kujisajili ili kuweza kupata taarifa za kila siku za klabu hiyo kwa njia ya mtandao.
Anasema pia watatumia maonesho hayo kukusanya takwimu mbalimbali za wanachama wao ili kuwapa fursa kujibu maswali ya wanachama hasa yale yanayowahusu wachezaji.
"Ndani ya banda letu wanachama wetu watapata fursa ya kununua jezi original kabisa za Yanga, lakini pia wakijisajili watakuwa wakipata habari za uhakika na hiyo itawasaidia kuachana na habari za mitandao ambazo nyingi zinakuwa sinza kweli," anasema Bumbuli.
Naye Kiungo mkabaji na Nahodha wa Yanga, Papy Tshishimbi anasema alikuwa nje ya timu baada ya kupata maumivu ya miguu ila kwa sasa wanaendelea vizuri na ataungana na wachezaji wenzake katika mazoezi.
Anasema anawaomba wanachama wa klabu hiyo waendelee kuisapoti timu yao kwani wanapofanya hivyo wanawatia moyo.
Aidha Tshishimbi amewataka wachezaji wenzake kuacha kusikiliza mambo ya mtandaoni bali washikamane na kushirikiana ili kuepuka utokeaji wa ugomvi.
"Timu haiwezi kujengwa na mchezaji peke yake bali kupata sapoti kutoka kwa wanachama na viongozi hivyo tunazidi kuwaomba waendelee kutusapoti," anasema

No comments:
Post a Comment