Wito huo ameutoa leo wakati wa ziara ya Bodi ya maji ya Taifa kukagua hatua mbalimbali zinazofanywa na wadau wa sekta ya maji katika kulinda na kuendeleza vyanzo vya maji nchini ziara ambayo imefanyika mkoani Tanga.
Amesema wananchi ni wadau muhimu katika
kufanikisha zoezi la utunzaji na uendelezaji wa vyanzo vya maji iwapo tu
wataelimishwa na kupewa njia mbadala itakayowawezesha kujikimu kimaisha badala
ya kuwabana kwa kutumia sheria peke yake.
“Kama tunataka kutunza mazingira yetu ili yawe endelevu isiwe tu kutumia sheria kuwabana wananchi bali waelimishwe na kupewa njia mbadala ya kujiongezea kipato ambayo vilevile inaweza kuwa inasadia kutunza mazingira.”
Awali akikagua Bwawa la ufugaji wa samaki
katika Kijiji cha pande Halmashauri ya Jiji la Tanga Afisa Maendeleo ya Jamii
Jiji la Tanga Bi. Zuwena Kilavu amesema Jiji hilo limewezesha kupunguza kwa
kiasi kikubwa uharibifu wa maji katika Mto zigi ambao ni tegemeo kubwa kwa wananchi
baada ya kuwaelimisha wananchi na
kuwajengea Bwala Kijiji hapo.
“Wananchi walikuwa wakichimba mchanga katika mto Zigi hali ambayo ilikuwa ikisababisha uharibifu mkubwa wa mazingira, baada ya kuwajengea Bwawa hili uharibifu umepungua sana na unaelekea kuisha kabisa. Amesema Zuwena.
Kwa upande wao wananchi wa Pande wameishukuru serikali kwa kuwajali na kwamba walikuwa wakipambana na hatari nyingi wakati wa kutafuta mchanga mtoni.
No comments:
Post a Comment