HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 28, 2020

Wafikishwa mahakamani wakidaiwa kuimba Bilioni 2

Na Janeth Jovin

Watu watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu  ikiwemo ya wizi na utakatishaji wa  zaidi ya Sh bilioni mbili mali ya Benki ya NMB.

Washtakiwa hao ni Joseph Nicas (63) Mlinzi na Mkazi wa Kimara, Paston Pangaja (37) Mkazi wa Mbeya na Jacob Mwakyembe (45)  dereva ambao wameunganishwa na washtakiwa wengine 20.


Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni ndugu watano Manjestus Mselema (44), Bernadetha  (45) ambaye ni mama wa nyumbani na Mkazi wa Mbagala, Agnes  (29) hotelia, Oswald Mselema (49) na Olaph Mselema (35) wote ni walinzi.

Walinzi wengine ni Beda Mkali (51) ambaye ni CTI Control, Kais Nasibu (35), John Selestine (45), Edes Hyera (43), Engelbert Masare (45), Bernad Victor (39) na Sylidion Odil (42).

Pia wapo Tulipo Mwamuzi (40) ambaye ni dereva, Grace Komba (32) Hotelia, Janeth Shilla (59) Wakala wa Kampuni ya Eternal International Ltd, Godwin (52) Fundi Mwashi na Anold Erio (25), Florah Mwita (25) mfanyabiashara na  Tispo Mwasakieni (27) maarufu Ronic Kinyozi na mkazi wa Kawe.

Akisoma hati ya mashtaka hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,  Yusto Ruboroga, Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono alidai washtakiwa hao na wenzao wanadaiwa katika tarehe tofauti mwaka 2020, maeneo ya Dar es Salaam washitakiwa Manjestus, Mwakuzi, Godwin, Anold, Agnes, Mwita, Victor na Odil walikula njama ya kuongoza genge la uhalifu kufanya kosa la wizi.

Ngukah alidai Juni 8,2020 maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washitakiwa wote waliiba Sh 2,082,000,000 mali ya Benki ya NMB.

Katika shtaka la tatu inadaiwa Juni 8,2020 maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, washitakiwa wote walijipatia Sh 2,082,000,000 mali ya NMB wakati wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa la wizi.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo, aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kukamilisha upelelezi.

Hakimu Ruboroga aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 11, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wote wamerudishwa rumande kwa sababu mashitaka yanayowakabili hayana dhamana kisheria.

No comments:

Post a Comment

Pages