Mwekahazina wa Kikundi cha Wakata Mkaa Happiness Mapunda akielezea waandishi wa habari namna wanavyotumia msiti kwa njia endelevu.
Waandishi na wanakijiji wa Kijiji cha Kitunduweta wakiwa ndani ya msitu wa kijiji unaohifadhiwa kwa njia USMJ.
Ofisa Sera na Majadiliano wa MJUMITA, Elida Fundi akielekea msituni katika kijiji cha Kitunduweta kujionea namna uhifadhi unavyotekelezwa.
Na Suleiman Msuya
WANAVIJIJI
wanajishughulisha na Usimamzi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (UMSJ),
wamesema bei elekezi iliyotolewa na Serikali katika biashara ya mkaa na
kubadilika kwa mfumo wa usajili kuhusu biashara hiyo umechangia miradi
mingi kusimama.
Kauli
hizo zimetolewa mbele ya waandishi wa habari hivi karibuni na wanavijiji
ambao wanajihusisha na uvunaji endelevu wa rasilimali misitu katika
vijiji vya Msolokelo, Matuli, Ulaya Mbuyuni na Kitunduweta vilivyopo
wilaya za Morogoro, Mvomero na Kilosa mkoani Morogoro
Waandishi
wa habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali walitembelea vijiji hivyo
kujionea namna USMJ kupitia Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya
Mkaa Tanzania (TTCS) chini ya uratibu wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya
Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Usimamizi wa Misitu ya Jamaii
Tanzania (MJUMITA) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC).
Jumanne
Omary Mkazi wa Kijiji cha Msolokelo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro,
alisema mradi wa TTCS umeweza kubadilisha maisha ya wananchi na kijiji
kupata maendeleo hivyo unapaswa kuendelezwa ila changamoto anayoiona ni
mfumo mpya wa usajili ili kupata kibali cha kuvuna mazao ya misitu.
Omary alisema mbaya zaidi mabadiliko hayo ya uvunaji yamekuja bila kuwashirilisha jambo ambalo limekwamisha mipango yao mingi.
"Sio
kwamba tunapinga mfumo mpya ila kusema kweli haukuwa shirikishi hali
ambayo imesimamisha mipango yetu ambayo tulijiwekea kwa mwaka 2019/2020,
nadhani wahusika wanatakiwa kutafakari upya," alisema.
Alisema
mwanya huo wa kuwanyima kupanga mipango ya uvunaji katika ngazi ya
kijiji inaweza kuchochea uharibifu mkubwa wa misitu hivyo ni vema
mamlaka husika kurejea mfumo wa zamani.
Omary
alisema pamoja na manufaa ambayo wamepata bado kuna changamoto ambazo
zinasababishwa na vijiji jirani vya Digarama, Masimba na Gonja ambao
wanavamia misitu yao na kuharibu.
Alisema
iwapo hakutakuwa na hatua za haraka kudhibiti wavamizi na kubadili
mfumo vijiji vyao havitahusika na uchumi wa kati unaozungumziwa.
Kwa
upande wake Sadick Kondo wa Kijiji cha Matuli, Kata ya Matuli wilayani
Morogoro, alisema mfumo huo umesimamisha shughuli za uvunaji jambo
ambalo linawarudisha nyuma kimaendeleo.
Kondo
alisema mwamko wa ulinzi na usimamizi wa misitu ya asili kijijini
unaanza kushuka baada ya mabaliko hayo ya mfumo wa usajili na bei
elekezi.
"Tulishajenga
imani moja kuwa misitu ni uhai wetu, tuitunze, tuitumie kiendelevu
lakini kwa hali ilivyo naona dalili mbaya tunapaswa kuchukua hatua
mapema," alisema.
Naye
Happiness Mapunda Mwekahazina wa Kikundi cha Wakata Mkaa Kitunfuweta,
Kata ya Muhenda wilayani Kilosa, alisema dhana ya usawa iliashaanza
kuonekana kijijini kwao lakini inaweza kurejea kwa kuwa wananchi
watakosa nguvu ya usimamizi wa misitu kwa kuwa hawana mamlaka kupanga
matumizi na bei.
Kulangwa
Ganda Katibu wa Kikundi cha Wakata Mkaa kijiji cha Kitunduweta, Kata ya
Muhenda wilaya ya Kilosa alisema haoni sababu ya Serikali Kuu kuchukua
jukumu la kupanga bei kwani wanaoumia ni wao.
Ganda alisema kupanga bei moja kwa nchi nzima kutanufaisha baadhi ya waandishi huku kundi kubwa likiathiriwa.
"Sio
ni mantiki ya kupanga bei elekezi ya mkaa kuwa shilingi 12,500 nchini
kote wakati kuna changamoto za usafiridhaji na zingine nyingi ambazo
zinahitaji ufumbuzi kwanza," alisema
Wakizungumzia
mfumo na bei elekezi Maofisa Misitu na Maliasili wa wilaya hizo
walisema zipo faida na hasara hivyo wao watajikita kwenye hasara ili
kuenda sawa na wanavijiji wanaotekeleza USMJ kwa vitendo.
John
Mtimbanjayo Ofisa Maliasili wa Wilaya Kilosa, alisema utulivu wa wilaya
ya Kilosa ni moja ya matunda chanya ya USMJ hivyo watahakikisha
wanapigania changamoto hizo zinapata majibu sahihi.
Naye
Edward Kimweri alisema Jamii inapaswa kujikita kwenye uhifadhi matokeo
makubwa na kuachana na hasara ambazo zimekuwa zikiwakwamisha.
Ofisa
Uhusiano wa TFCG, Bettie Luwuge alisema wao wameamua kujikita kwenye
uhifadhi wakiamini kwa ni eneo rahisi kuchochea maendeleo.
Luwuge alisema mradi wa mkaa endelevu kuhakikisha kuwa Misitu ipo salama ma mazingira kwa kila jambo.
No comments:
Post a Comment