Na Mwandishi Wetu
BAADA ya kuahirishwa kwa Tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2020 ambalo lilipaswa kufanyika Agosti 23 sasa ni rasmi litafanyika September 6 Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kuelekea Tamasha hilo Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, amesema utaratibu wa Tamasha utabaki kama ulivyopangwa kufanyika hapo awali kwamba Tamasha hilo halina kiingilio litakuwa ni Tamasha la bure.
“Tamasha letu la kuombea Uchaguzi lilikuwa lifanyika Agosti 23 jijini Dar es Salaam lakini tumeliahirisha kama ambavyo nilivyosema. Na Tamasha hilo sasa litafannyika Septemba 6 palepale katika Uwanja wa Uhuru.
“Utaratibu wetu ni uleule kwamba Tamasha hilo halina kiiingilio, litakuwa ni Tamasha la bure, wewe ni kuchukua familia yako na kuja nayo katika Tamasha hilo la kuombea Uchaguzi, wapo waimbaji mbalimbali ambao tumewatangaza, na kama mnavyoona leo tunae Rose Muhando, na waimbaji wengine ni wale wale kama ambavyo tulikuwa tumetangaza hapo awali.”amesema Msama.
Msama amewataka watanzania kujiandaa kwa ajili ya Tamasha hilo, kwani Msama Productions imekaa muda mrefu pasipo kuandaa Taamasha lolote, hivyo wajitokeze kushuhudia kitakachojiri siku hiyo.
Kwa upande wa Rose Muhando amesema yuko tayari kuwasha moto katika siku hiyo adhimu ya kuliombeea Taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa U Rais, Ubunge na U Diwani 2020.
“Kama mnavyoniona nitakuwepo kuwasha moto juu ya moto yaani moto ‘fire’ kama kawaida yangu hakuna kupoa hakuna kulala, maana Mungu pia ninaye mwabudu na kumtumikia yeye hajawahi kulala wala kusinzia mimi nawezaje kulala, na tunawezaje kulala katikati ya wimbi hili la Uchaguz?.
“Kwa hiyo tutakuwa na hilo Tamasha la Septemba 6 kwa ajili ya kusimika Madhabahu yetu ya kiongozi wetu kwa ajili ya kuongoza nchi yetu tena, kwaiyo nitakuwepo nimejipanga vizuri sana Watanzania tujitokeze kwa ajili ya kumkabidhi Mungu Uchanguzi Mkuu.”amesema Mhando.
No comments:
Post a Comment