Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu, akionesha llani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kumpokea mgombea Urais wa chama hicho Dkt. John Magufuli ambaye anatarajia kuwasili mkoani hapa kesho.
Mabango yenye picha za mgombea huyo yakiwekwa Barabara Kuu ya Singida Dodoma.
Watoto Ashiruna Athumani (kushoto) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Utemini mkoani hapa na wadogo zake wakitazama picha ya mgombea huyo iliyoweka viwanja vya Bombadia.
Vijana wa Jeshi la Akiba wakisafisha eneo la uwanja utakapofanyika mkutano wa mgombea huyo.
Uwanja utakapofanyika mkutano huo.Mabango yenye picha za mgombea huyo yakiwa yamewekwa Barabara Kuu ya Singida Dodoma.
Mafundi wakiendelea na kazi ya kusimika Jukwaa utakapofanyika mkutano huo.
Mafundi wakiendelea na kazi ya kusimika Jukwaa utakapofanyika mkutano huo.
Wajasiriamali wakichangamkia fursa ya mkutano huo kwa kuuza sare za chama hicho.
Na Boniphace Jilili na Dotto Mwaibale, Singida
MAANDALIZI ya kumpokea mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Singida Dkt John Pombe Magufuli yanaendelea kukamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi hayo Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Ahmed Kaburu alisema maandalizi yanaendelea kukamilika ambapo kesho wanatarajia kumpokea Mgombea huyo mkoani hapa.
Kaburu alisema mgombea huyo ataongea na wananchi wa Mkoa huo kwenye viwanja vya Bombadia vilivyopo Manispaa ya Singida.
"Kesho majira ya saa nne asubuhi nawakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Singida mfike kwenye viwanja vya Bombadia kuja kumsikiliza Dkt John Pombe Magufuli mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chetu cha CCM." alisema kaburu.
Alisema pamoja na maandalizi yote mgombea huyo atahutubia wanachama na wananchi pamoja na kunadi ilani ya chama hicho ya mwaka 2020-2025 ambayo alisema imejaa shehena ya vitu vizuri,pia atapata fursa ya kuwatambulisha na kuwanadi wagombea nafasi ya ubunge katika majimbo nane ya mkoa huo.
Katika mkutano huo wamekaribishwa wazee maarufu, viongozi wa dini pamoja na wasanii mbalimbali watakaotoa burudani.
No comments:
Post a Comment