Mshindi wa kura za maoni Ubunge viti maalumu kundi la Wazazi mkoa wa Kilimanjaro Ester Rwegasha akiwa ameshikilia namba yake wakati akiomba kura kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Kilimanjaro.
Wagombea wa nafasi ya Ubunge Viti Maalumu kundi la Wazazi mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wameshikilia namba zao wakizonesha mbele ya Wajumbe (hawapo pichani) wakati wa kuomba kura ,kutoka kulia ni Zaina Heshima,Tusajigwe Ngwira ,Luisivivy Machange,Florance Sawe na Ester Rwegasha .
Wajumbe kutoka wilaya ya Moshi vijijini wakipiga kura.
Wajumbe kutoka wilaya ya Same wakipiga kura.
Msimamizi wa Uchaguzi ,Jonathan Mabiya akihesabu kura zilizopigwa huku Wagombea wakishuhdia zoezi hilo.
Mshindi wa kura za maoni Ubunge viti maalumu kundi la Wazazi Ester Rwegasha akitia saini fomu za matokeo mara baada ya kuongoza katika kura za maoni .
Mshindi wa kura za maoni Ubunge viti maalumu kundi la Wazazi mkoa wa Kilimanjaro Ester Rwegasha (kushoto) akiwa na mshiriki aliyeshika nafasi ya pili baada ya kumshinda kwa kura moja pekee Tusajigwe Ngwira .
Mshindi wa kura za maoni Ubunge viti maalumu kundi la Wazazi mkoa wa Kilimanjaro Ester Rwegasha (kushoto) akiwa na wagombea wengine mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uchaguzi kwa jumuiya hiyo.
Na Dixon Busagaga, Kilimanjaro
JUMUIYA ya Wazazi wa
Chama cha Mapinduzi imefanya chaguzi za kura za maoni ikiwa ni mara ya kwanza kwa
Jumuiya hiyo kupata uwakilishi wa Wabunge wa viti maalumu katika Bunge la
Jamhuri ya muungani wa Tanzania ambapo kwa Kilimanjaro Mjane Ester Rwegasha ameshinda
nafasi hiyo.
Nafasi ya Ubunge
Vitimaalumu kupitia jumuiya ya Wazazi kwa mkoa wa Kilimanjaro imegombewa na
makada Sita wa Chama cha Mapinduzi huku wajumbe 38 wa mkutano mkuu wa Jumiya ya
Wazee mkoa wa Kilimanjaro wakifanya maamuzi ya kupata mwakilishi wa jumuiya
hiyo.
Waliojitokeza kugombea
nafasi hiyo ambayo baadae atashindanishwa na washindi wengine kutoka mikoa 31
ya Tanzania bara ni pamoja na Zaina
Heshima ,Luisivivy Machange ,Flora Mbaga ,Florance Sawe ,Tusajigwe Ngwira na Ester
Rwegasha.
Msimamizi wa Uchaguzi ,Jonathan
Mabiya alimtangaza Ester Rwegasha
kuongoza katika zoezi la kura za maoni baada ya kupata kura 18 akimpita kwa
kura moja mshindani wake Tusajigwe Ngwira aliyepata kura 17.
Katika kura za awali
Ester Rwegasha na Tusajigwe Ngwira walifungana baada ya kila mmoja kupata kura
15 kati ya kura 38 zilizopigwa hali iliyomlazimu msimamizi wa Uchaguzi ,Mabiya
kutangaza awamu nyingine ya upigaji kura kwa wawili hao.
“Walioudhuria ni 38 na
kura zilizopigwa ni 38 ,hakuna kura iliyoharibika ,kura halali zikawa 38 ,Zaina
Shabani Heshima amepata Sifuri,Luisivivy Machange amepata Sifuri, Flora Mbaga amepata
kura 1, Florance Mushi amepata 7,na wafuatao kwa pamoja walifungana ,Tusajigwe Ngwira
15 na Ester Rwegasha 15.”alitangaza Mabiya.
Akizungumza mara baada
ya kutangaza matokeo Jonathan Mabiya ambaye pia ni katibu wa Chama cha
Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro alisema Kilimanjaro anapelekwa mtu atakaye kuwa
mbunge kupitia jumuiya hiyo.
“Tutaenda Dodoma kwa
wingi ili Kilimanjaro ipate mbunge wa kundi la Wazazi ,kule taifa wazazi wana
nafasi mbili mbili, moja kutoka Zanzibar na moja kutoka bara ,sasa hiyo moja tupeleke mtu
ambaye watasema kweli Kilimanjaro imeleta mshindani na sio mshiriki.”alisema
Mabiya .
Mshindi wa kura za
maoni kupitia Jumuiya ya Wazee mkoa wa Kilimanjaro Ester Rwegasha aliyefiwa na
mumewe miaka mitatu iliyopita kwa ugonjwa wa Saratani ya Tumbo alisema yapo
mengi yamemgusa katika jumuiya ya Wazazi na kwamba huu ndio muda wa
kuyatekeleza.
“Nimekuwepo katika Jumuiya
yetu hii ya wazazi, nikiwa kama mwalimu yapo mambo ambayo nimeyaona yamegusa
moyo wangu sana kiasi cha kuumia ,nina kili mbele yenu mimi ni mzalendo wa nchi
yangu.na nina ipenda sana nchi yangu”alisema Rwegasha.
“Mbali na maujukumu
ambayo ninayo ya kila siku nimedhamiria kutoka kwenye kilindi cha moyo wangu
,nimekuja kwenye Jumuiya yetu hii ya wazazi ,ili tuweze kushirikiana pamoja
tuzifufue shule zote ambazo zimekufa,na zile ambazo hazifanyi vizuri”aliongeza
Rwegasha
Suala la kubuni miradi
ni miongoni mwa masuala ambayo Rwegasha amelipa kipaumbele huku akiweka mkakati
kwa wilaya zisizokuwa na miradi kwa jumuiya ya Wazazi kupata miradi ili
kuongeza kipato kwa jumuiya hiyo.
“Nina nguvu nina uwezo
wa kukimbia huku na kule ,mimi ni jasiri an naomba mniamini mnitume popote na nitakwenda
kuwawakilisha vyema.” Alisema Rwegasha.
No comments:
Post a Comment