NA JANETH JOVIN
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeitaka Kampuni ya Raha Limited ambayo inatoa huduma za mawasiliano kulipa faini ya Sh bilioni 11.89 kwa kukiuka sheria, kanuni, taratibu na masharti ya leseni za mamlaka hiyo
Katika fedha hizo, Kampuni ya Raha inatakiwa kutoa Sh 11,850,000 kwa kutumia masafa ya mawasiliano ya redio katika wigo wa 1452-1482 MHZ bila leseni kutoka TCRA tangu Machi mwaka huu.
Hayo yalibainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa TCRA, James Kilaba wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya ukaguzi kwa kampuni hiyo na kubaini makosa mbalimbali.
Kilaba amesema masafa ni rasilimali adimu ya taifa ambayo hayakopeshwi wala kuibwa hivyo, kama mtu anataka kuyatumia masafa hayo anapaswa kuomba leseni.
Amesema tangu Machi mwaka huu kampuni hiyo imekuwa ikitumia masafa hayo bila leseni halali na kwamba kuhusu gharama hiyo, waangalie kisheria ni kiasi gani kwa siku ambacho wamenufaika kwa kutumia masafa hayo.
Mkurugenzi huyo amesema makosa mengine iliyoyabaini ni kampuni hiyo kushindwa kujenga, kusimika, kuendeleza, kusimamia na kuwezesha upatikanaji wa miundombinu ya mawasiliano Mkoa wa Tanga kwa kujibu wa leseni yake hiyo itatakiwa kulipa faini ya Sh milioni tano.
Pia kampuni hiyo itatakiwa kulipa faini ya Sh milioni 10 kwa kujenga miundombinu ya mfumo wa mawasiliano, kuendesha na kutoa huduma za mawasiliano mkoani Mtwara bila leseni ya TCRA.
Hivyo, Kampuni ya Raha imetakiwa kulipa faini ya Sh milioni tano kwa kutotimiza masharti ya leseni baada ya kushindwa kutoa huduma mkoani Kagera Agosti 2019.
"Kampuni ya Raha itatakiwa kulipa faini ya Sh milioni tano kwa kushindwa kuwasilisha kwa TCRA taarifa za ukaguzi wa mahesabu yake ndani ya miezi sita kuanzia mwaka wa fedha, kulipa faini ya Sh milioni tano kwa kushindwa kuwasilisha kwa mamlaka mpango mkakati wa mwaka wa kuendeleza rasilimali watu na inatakiwa kulipa faini ya Sh milioni 10 kwa kushindwa kutimiza masharti ya leseni, hususan kushindwa kuhuisha leseni kwa muda uliopangwa," amesema Kilaba.
Alifafanua kuwa kampuni hiyo ilipewa leseni ya kujenga, kusikika, kutunza na kusimamia miundombinu ya mawasiliano katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Tanga ifikapo Februari mwaka huu na Kilimanjaro ifikapo Septemba mwaka huu.
Amesema walikuwa na jukumu la kuandaa na kuwasilisha kwa TCRA mpango wa kuendeleza rasilimali watu, kuandaa na kuwasilisha namna mpango huo uliowasilishwa unavyotekelezwa kila mwaka na kuwasilisha kila mwaka namna inavyosambaza huduma zake kwenye eneo alipangiwa na idadi ya watu aliowafikia.
Mkurugenzi huyo alieleza kuwa walitoa leseni kwa Kampuni ya Raha ili kutoa huduma za mawasiliano kitaifa kwa mikoa ya Mara, Kagera na Manyara.
Vilevile, iliwataka kuhuishwa kwa leseni miezi 12 kabla ya kumalizika kwa muda wa leseni ambazo zimetolewa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Machi 24,2015 na kuipatia TCRA taarifa za mahesabu yaliyojadiliwa ndani ya miezi sita baada ya kumalizika kwa mwaka wa fedha na kuandaa kila mwaka mpango wa maendeleo ya rasilimali watu na utekelezaji wake.
August 29, 2020
Home
Unlabelled
TCRA yaitoza faini ya Bilioni 11.8 Kampuni ya Raha Limited
TCRA yaitoza faini ya Bilioni 11.8 Kampuni ya Raha Limited
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment