Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, amezungumzia changamoto zinazojitokeza kwenye Uchaguzi Mkuu zinazosababishwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa.
IGP Sirro aliyasema hayo jijini Dar es Salaama wakati wa Mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwa vyama vya Siasa na wadau wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020 ambao uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC), alisema jeshi hilo limejipanga kuwashughulikia wanasiasa watakao vunja amani.
Alisema jeshi
hilo limekuwa likibainia kuwepo kwa wanasiana amesema jeshi hilo limejipanga kuwashughulikia wahalifu na wanasiasa watakaokwenda kinyume na taratibu na waliopanga kufanya vurugu kabla ya uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28,2020.
Alisema jeshi la polisi linaendelea na mafunzo ya utayari kwa vikosi maalum ikiwemo vikosi vya kutunza ghasia, mbwa,farasi nchi nzima ambavyo vitaongeza nguvu kutoa msaada wa haraka ili kukabiliana na vitendo vyenye nia ya kuvuruga usalama, Amani utulivu wakati wa kufanya kampeni, uchaguzi, utangazaji wa matokeo ,kuapishwa kwa viongozi na baada ya uchagzi kumalizika.
Alisema Amani ya nchi ni muhimu kuliko kitu chochote duniani na bila Amani na utulivu hakuna siasa hivyo wanasiasa wanapaswa kufanya siasa zenye mihemko ambazo zitasababisha nchi kuingia kwenye vurugu.
“Vurugu haziwezi kukuingiza madarakani, wananchi wanataka kusikiasera, kujua unawafanyia nini ukiingia madarakani na si matusi pamoja na kufanya vurugu kwa viongozi wenzako. Hasira huondoa busara na kuleta maafa, je watu wakifa wewe utapata faida gani? Kama unataka kufa kwa ajili ya kutaka uongozi Je ukifa utamuongoza nani?” alihoji Sirro.
IGP Siro aliongeza kuwa Jeshi la Polisi limejipanga kusimamia sharia, kanuni, na taratibu za uchaguzi ili kuhakikisha kuna usalama, Amani na utulivu wakati wote wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwakamata nakuwafikisha mahakamani wote watakaokwenda kinyume na sheria.
Aidha aliwaasa viongozi wa vyama vya siasa kutoingilia majukumu yajeshi hilo na badala yake wajikite kufanya siasa safi zisizo za uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake Msajili wa Vyama vya siasa, Jaji Mstaafu Fransic Mutungi aliwataka wanasiasa kutotumia mitandao ya kijamii, vyombo vya habari kupotosha umma wakati jambo si kama lilivyo na kuwapa hofu wananchi na jamii kwa ujumla.
“Kuna viongozi wameingia kwenye mtandao wa kijamii wa Tweeter wanaanza kueleza kwamna Ofisi ya Msajili haijasambaza fomu …wasiharakishe kuanza kutia hofu jamii maana hiyo ilikuwa taswira mbaya sana kana kwamba kuna kitu kwa nini wanacheleweshewa wakati si kweli, bahati mbaya nimekuja kwenye kikao hiki hawapo ili hata wapate majibu sahihi ya jambo hilo.
Akitoa mada ya sharia ya gharama za uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alisema sheria hiyo inadhibiti matumizi ya fedha katika uchaguzi kwa kuweka ukomo wa matumizi na kuweka sharti la kutoa taarifa juu ya mapato na matumizi ya gharama za uchaguzi.
“Sheria inadhibiti kuingiza gharama za uchaguzi kutoka nje ya nchi kabla ya miezi mitatu na kuitolea taarifa Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa,”alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, alisema uchaguzi unapaswa kuwa wa amani kwa kuzingatia uongozi na utawala unaozingatia katiba, sheria zinazotungwa hasa za uchaguzi nakanuni zote, utaratibu na maadili.
Alisema habari za uongozi katika taifa hili hazikuanza leo, ambapo historia inaonesha vyama si mali ya umma wala mtu binafsi bali ni vyawananchi.
Butiku alisema kuwa kiongozi atakayepewa nafasi kuongoza chama ujue si mali yako,CCM si mali yake bali ni ya wananchi wote ama wanachama bali amepewa heshima ya kuongoza chombo hicho uongozi ni dhamana tuu si mali.
“Mfano Chadema si mali ya umma wala CCM, bali ni mali ya watanzania vimeundwa ili viwahudumie watanzania na vipo ndani ya katiba na kupewa nafasi maalumu ya kusimamia siasa ya nchi ni nafasi ya heshima, “alisema.
Mwenyekiti Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu), Semistocles Kaijage, alisema mchakato wa uchukuaji fomu kugombea nafasi ya Urais unaendelea ambapo hadi sasa wagombea 17 wamejitokeza kwa nafasi za urais.
No comments:
Post a Comment