HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 03, 2020

USHAURI WA KISHERIA BURE KWA WANANCHI WANAOTEMBELEA MAONYESHO YA NANENANE MBEYA

Mkuu wa Kampasi ya Mbeya Prof. George Shumbusho (katikati kushoto) akipokea maelezo kuhusu mwenendo mzima wa maonyesho tangu yalipoanza tarehe 01Agosti, 2020. kutoka kwa mmoja wa washiriki wa maonyesho hayo Bw. John Jorojick.
Mkuu wa Kampasi akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa washiri kuhusu nasuala ya Programu na maswali ya jumla toka kwa wananchi.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Maghabe ya mjini Mbeya, wakipata maelezo ya kina kuhusu shughuli za Chuo Kikuu Mzumbe walipotembea Banda la Maonyesho Nanenane viwanja vya John Mwakangale Mbeya.
Mkuu wa Kampasi ya Mbeya Prof. George Shumbusho akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampasi hiyo (wenye sare) wanaoshiriki maonyesho ya Nanenane kwenye viwanja vya John Mwakangale Mbeya.


Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya, kinatoa mafunzo na ushauri wa kisheria bure kwa wananchi wanaoshiriki maonyesho ya mwaka huu ya Nanenane kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Akizungumza kuhusu Maonyesho hayo; Mkuu wa Kampasi hiyo Profesa George Shumbusho amesema mbali na kutoa mafunzo ya Ujasiriamali na ushauri wa Sheria, Chuo hicho pia kina maonyesho ya bidhaa za wanafunzi ambao wamepata mafunzo ya ujasiriamali chuoni hapo, pamoja na kutoa elimu ya kozi zinazotolewa na chuo hicho kwa ngazi ya Stashahada,
Shahada za Kwanza na Shahada za Uzamili.

“Mwitikio wa watu ni mkubwa na wengi wakitaka kufahamu namna ya kuendesha biashara na shughuli za ujasiriamali kwa jumla, namna ya kuandika mikataba, uanzishaji wa vikundi
n.k… watalaamu wa Sheria pamoja na Shule ya Biashara wapo na watakuwepo kwa siku zote za maonyesho haya kuwasaidia wananchi ambao wanatoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
kutembelea maonyesho ya Nanenane”. Alisisitiza.

Akifafanua zaidi namna gani wanavyoendesha mafunzo ya Sheria kwa wananchi, Mratibu wa maonyesho hayo ambaye pia ni mtaalamu wa Sheria kutoka Kitivo cha Sheria cha Chuo
Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya, Bw. John Steven amesema wameandaa darasa ambapo wananchi kwakuwa wanafika kwa wingi hupatiwa mafunzo kwa ujumla na pale inapohitaji
msaaada zaidi kwa mmoja mmoja wamekuwa wakifanya hivyo ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kuandika mikataba bure.

Maonyesho ya Nanenane kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanaendelea katika viwanja vya John Mwakangale Mbeya, na kushirikisha mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Katavi, Iringa,
Songwe, Rukwa na Njombe.

No comments:

Post a Comment

Pages