Na Zuena Msuya, DSM
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Leonard Masanja amesema haridhishwi na kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji wa umeme katika Vijiji vilivyo pembezoni mwa Mji (Peri Urban)katika Mkoa wa Pwani.
Mhandisi Masanja alisema hayo katika ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo katika Wilaya ya Kisarawe, Kibaha, Bagamoyo na Mkuranga mkoani Pwani aliyoifanya Agosti 8-9, 2020 mkoani humo.
Mara baada ya kutembelea mradi huo na kuona hali ya utekelezaji, Mhandisi Masanja alisema kuwa haridhishwi na kasi ya utekelezaji wa mradi huo kwakuwa wakandarasi wote waliopewa dhamana ya kutekeleza mradi huo wapo chini ya kiwango cha utekelezaji kulingana na makubaliano ya mkataba.
“Siridhiswi na kasi ya utekelezaji wa mradi huu , vilevile hawa wakandarasi wote wanaotekeleza mradi huu wa Peri Urban wako chini ya kiwango cha makubaliano ya mkataba,pia hakuna hata mmoja aliyefikisha asilimia 50 mpaka sasa ya kuunganisha wateja anaotakiwa kuwaunganisha, mradi huu unatekelezwa kwa miezi tisa kuanzia Desemba mwaka jana, utakamilika mwanzoni mwa mwezi ujao( Septemba), mpaka sasa wamebakiwa na siku chache sana na wanakazi kubwa, watu wa namna hii hatuwezi kuwavumilia hali ya kuwa Serikali imekuwa ikiwalipa fedha zao bila vikwazo vyovyote alikemea Mhandsi Msanja.
Aidha aliweka wazi kuwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya usambazaji wa umeme vijijini wengi wao wamekuwa wakitumia fedha wanazolipwa kufanya mambo mengine badala ya kuelekeza fedha hizo katika miradi husika hivyo kusababisha wengi kushindwa kukamilisha miradi hiyo kama ilivyopangwa kwa kukosa fedha,wakati tayari serikali imekwishawalipa fedha za utekelezaji mradi.
Vilevile , aliwataka wakandarasi wote nchi wanaotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kuhakikisha kuwa fedha wanazolipwa kwa ajli ya kufanya kazi hizo wafanye kwanza kazi kusudiwa na ndipo waendelee na mambo mengine ili kuondokana na changamoto ya kukosa fedha za kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
“Nimebaini kuwa, wakandarasi wengi wamekuwa wakitumia fedha za miradi kufanya mambo yao binafsi badala ya mradi husika akitegemea kuwa atapata fedha sehemu nyingine na kuja kuendelea na mradi, hii jambo si sahihi linasababisha kazi kuchelewa,kodorora ama kusuasua, vilevile kujengwa kwa kukimbizana na muda, jambo ambalo wakati mwingine linasababisha ijengwe chini ya kiwango cha ubora unaotakiwa, ni vyema mkandarasi akatumia fedha katika kazi husika na kwa kufanya hivyo atafanya kazi zake kwa wakati, na kwa ubora, hii itamjengea uaminifu na fursa nyingi za kupata kazi kubwa zaidi, alisisitiza Mhandisi Masanja.
Katika Mkoa wa Pwani Wakandarasi wanne wamepewa jukumu la kutekeleza mradi wa Peri Urban ambao ni Kampuni ya Namis wanaotekeleza katika Wilaya ya Kisarawe, Kampuni ya Sengerema wilayani ya Kibaha, Kampuni ya SinoTek wilayani Bagamoyo na Kampuni ya Ceylex wilayani Mkuranga, ambao wote hakuna aliyefikisha kiwango cha utekelezaji wa mradi kulingana na mkataba ambao unakamilika mwanzoni mwa mwezi Septemba.
Sambamba na hilo, aliwataka wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya kusambaza umeme kuzingatia sheria za barabara kwa kusimika nguzo maeneo sahihi ili kuondoa usumbufu wa kuhamisha nguzo hizo ikitokea barabara inatanuliwa.
Aliagiza, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuwasimamia kwa karibu wakandarasi hao na endapo kutakuwa changamoto ambazo zitaonekana kuwakwamisha kwa upande wa serikali, wazitatue haraka ili mradi huo ukamilike kama ilivyopangwa.
Kwa upande wao wakandarasi hao, wameahidi kukamilisha utekelezaji wa mradi huo kabla ya mwisho wa mwezi huu( Agosti) wakieleza kuwa wanavifaa vyote vinavyohitajika, pia wameongeza nguvu kazi na watafanya kazi zao usiku na mchana ili kukamilisha kazi hiyo kwa wakati kulingana na makubaliano ya mikataba.
Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu huyo aliahidi kutembelea tena mradi huo, mwishoni mwa mwezi huu (Agosti)ili kuona hatua zaidi za utekelezaji wa mradi huo kama walivyoahidi wakandarasi hao,kabla ya hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa.
Alisema kuwa, Serikali imekuwa ikitoa vipaumbele kwa kuwainua wawekezaji wazawa kutekeleza miradi ya ndani,na wengi wao wenye uwezo wamepata kazi nyingi, hivyo Serikali haitasita kuwanyima fursa ya kutekeleza miradi ya namna hiyo wawekezaji wazawa watakaoshindwa kufanya kazi zao kwa ubora na viwango vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na kumaliza kwa wakati kulingana na makubaliano ya mikataba.
Ikumbukwe kuwa, Naibu Katibu Mkuu huyo, alifanya ziara kama hiyo Julai 11,2020 na aliwaagiza wakandarasi hao kuongeza kasi ya kutekeleza mradi huo, baada ya kuona utekelezaji wake unasuasua, ili hadi kufikia mwishoni mwa Agosti, 2020 wawe wamekalisha mradi huo.
August 12, 2020
Home
Unlabelled
Utekelezaji wa Peri Urban Pwani hauridhishi
Utekelezaji wa Peri Urban Pwani hauridhishi
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment