Na Janeth Jovin
WAFANYABIASHARA wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, kwa kosa la kuingilia miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kujiunganishia umeme kinyume na sheria.
Wafanyabiashara hao ambao ni waarabu ni Ahmed Khalifa (40) Mkazi wa Mikocheni na Abdulrazak Saidi (49) Mkazi wa Temeke, Dar es Salaam walifikishwa mahakamani hapo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kassian Matembele wa Mahakama hiyo.
Akisoma hati mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Maternus Marandu akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Saimon na Wakili wa Serikali, Benson Mwaitenda amedai kuwa Julai 29,2020 washtakiwa wakiwa eneo la Mikocheni barabara ya Ndovu, Wilaya ya Kinondoni ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa makusudi waliingilia mali inayotoa huduma muhimu.
Wakili Marandu amedai kuwa washtakiwa hao walijiunganishia umeme kutoka katika mfumo wa Tanesco na kupitisha pembeni ya mita namba 43153725676 kinyume na sheria.
Akizungumza kuhusu hatua ya upelelezi, Wakili Marandu amedai kuwa upelelezi bado aujakamilika, lakini umefikia hatua nzuri, kwa hiyo wanaomba tarehe ya karibu kama wiki mbili, utakuwa umekamilika.
Hata hivyo, Hakimu Matembele amesema ili washtakiwa wawe nje kwa dhamana kila mmoja anatakiwa awe na mdhamini mmoja, ambae atakuwa na barua ya utambulisho na kitambulisho cha Taifa au cha kupigia kura.
"Washtakiwa pamoja na wadhamini wao watatakiwa kusaini fungu la dhamana la Sh. Milioni tano na pia hamtatakiwa kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kibali cha Mahakama, " amesema Matembele
Kesi imeahirishwa hadi Septemba 10, mwaka huu itakapokuja kwa kutajwa na kuangalia upelelezi umefikia hatua gani. Washtakiwa wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.Wafanyabiashara wawili kizimbani kwa kosa la kuingilia miundombinu ya Tanesco
August 27, 2020
Home
Unlabelled
Wafanyabiashara wawili kizimbani kwa kosa la kuingilia miundombinu ya Tanesco
Wafanyabiashara wawili kizimbani kwa kosa la kuingilia miundombinu ya Tanesco
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment