Bernard Morrison.
NA ABDALLAH HIJA
Mabingwa wa Kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), Yanga SC
imezuia kibali cha kazi cha Kiungo mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo
aliyejiunga na wapinzani wao Simba Bernard Morrison wakidai kuwa ni
mchezaji wao.
Hivi karibuni jiji lilizizima kufuatia sakata la mkataba wa Morrison na
Yanga huku wanajangwani wakidai bado wanammiliki nyota huyo.
Wakati Kiungo huyo mshambuliaji akidai kuwa hana mkataba na Yanga hali
iliyopelekea shauri lao kufika hadi kamati ya maadili na Hadhi za
Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) huku Morrison akiibuka
mshindi kwenye sakata hilo akiwapiga bao Wanajangwani.
Lakini kutokana na hilo jana Yanga, wamepeleka rufaa kwenye Mahakama ya
Michezo ya Kimataifa (CAS), huku wakizuia kibali cha kazi cha mchezaji
huyo hadi pale kesi hiyo itakapoamuliwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Ofisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli
alisema, wamepokea barua kutoka kwa Ofisa wa Wizara ya kazi kuhusu
kibali cha Morrison, wao wakamjibu bado ni mchezaji wao.
“Tulipokea barua kwa Ofisa mmoja wa Wizara ya kazi kuhusu kibali cha
Morrison, sisi tulimjibu kwamba yule bado ni mchezaji wa Yanga na hata
katika hukumu iliyotolewa ilionyesha mkataba una mapungufu na hayawezi
kufanya mkataba kuvunjika.
“Lakini kilichotushanagaza kwenye Wizara imekuwa na ‘interest’ na jambo
hili hasa kwa Morrison, kwanini ofisa huyu ametetea suala hili kwa
maneno makali kwamaba turejeshe kibali hicho” alihoji Bumbuli nba
kuongeza:
Kwa hiyo tutarejesha kibali hicho hadi shauri likiwa limekamilika na
sio kutushinikiza kwa sababu ambazo Ofisa amezitaka, Morisson ni
mchezaji wa Yanga bado tunaye sisi.
No comments:
Post a Comment