Mafunzo hayo
yaliyotolewa na maofisa kutoka CRDB Makao makuu na Kanda ya Kaskazini
yametolewa kwa mawakala kutoka maeneo ya Mwanga ,Himo ,Marangu ,Rommbo
Mkuu,Tarakea na Holili ikiwa ni muendelezo wa mafunzo yanayofanyika nchi nzima
.
Akifungua mafunzo hayo
katika Hoteli ya African Flower iliyopo mji mdogo wa Himo ,Mkuu wa mkoa wa
Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira alisema ni rahisi kwa wahalifu kujaribu kuwatumia
.
“Kupitia mafunzo haya
mazuri mtaweza kupewa elimu ya kumtambua mteja wako na kumuhudumia ipasavyo na
kukuwezesha kulinda na kukuza mtaji wako uweze kufanya kazi vyema zaidi.” Alisema
Dkt Mghwira .
Alisema uwakala wa
Kibenki umefungua Fursa nyingi na kuwezesha kukua kwa uchumi na kwamba serikali
inajivunia uwepo wa mawakala kwa kufungua milango ya urahisi wa kukusanya kodi
kwa kuwezesha wananchi kulipia kodi popote alipo kwa Wakala wa CRDB.
“Wakala wa CRDB ni
moja ya njia zinazoongoza kupendwa na wananchi kulipia kodi ambapo naambiwa zaidi
ya miamala millioni 8 yenye thamani zaidi ya Bil 300 zilikusanywa kupitia wakala
wa CRDB kwa Mwaka Jana tu.”alisema Dkt Mghwira
“Na kwa nusu ya mwaka
huu tayari mmesaidia serikali kukusanya
zaidi ya Bil 350..hii ni kidhihirisho kwamba uwakala wa CRDB ni
kichocheo kikubwa cha maendeleo ya Taifa kwa ujumla.”aliongeza Dkt Mghwira .
Naye Meneja wa CRDB
kanda ya Kaskazini ,Chiku Issa alisema CRDB
ndio benki ya kwanza kuanzisha huduma za mawakala wa benki ambazo ilianzisha mwaka
2013 na kwamba kwa sasa ina mawakala zaidi ya 16,000 waliotapakaa Tanzania
nzima.
“Moja ya lengo la
kuandaa semina hii ilikuwa kuwashukuru
mawakala hao katika kutambua mchango wao katika kukubali kushirikiana na benki
ya CRDB katika kupeleka huduma karibu na wateja lakini pia kuwajumuisha
wananchi kwenye huduma za kifedha (financial inclusion)”alisema Chiku
Alisema mawakala
wa CRDB wamesaidia kuongeza huduma za
kibenki kwa kuongeza muda wa wateja kufanya miamala ambapo baadhi ya mawakala
wanatoa huduma kwa masaa 24.
“Mafunzo haya yamelenga
pia kuwakumbusha mawakala kufuata taratibu na kanuni zote za kifedha kama
zinavyosimamiwa na benki kuu. Lakini pia wamepewa elimu kuhusiana na elimu ya
utakatishaji Fedha.”alisema Chiku.
CRDB imetoa elimu ya
ujasiliamali na njia nzuri zaidi ya kuhudumia wateja wa benki, pamoja na
kusaidia kuongeza wateja ili wananchi waendelee kufurahia huduma zetu lakini
pia na mawakala waweze kujipatia kipato zaidi.
No comments:
Post a Comment