Msimamizi wa ujenzi wa soko la Manispaa ya Morogoro Eng. Juma Gwisu akifafanua jambo kwa wahandisi kutoka Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), walipokagua maenedeleo ya ujenzi wa soko hilo.
Muonekano wa nje wa soko la kisasa la Manispaa ya Morogoro ambalo ujenzi wake umekamilika.
Msajili wa wahandisi Eng. Patrick Barozi akisisitiza jambo kwa wahandisi wanaosimamia ukarabati mkubwa wa machinjio ya kisasa katika ranch ya
Nguru Hills Mvomero mkoani Morogoro
Muonekano wa machinjio ya kisasa katika ranch ya Nguru Hills Mvomero mkoani Morogoro.
Ujenzi wa mifereji ya kupitisha maji kwenda kwenye mabwawa ya kumwagilia miwa katika shamba la miwa la Mbigiri ukiendelea, shamba hilo ni sehemu ya mashamba yanayomilikiwa na kiwanda cha sukari cha Mkulazi mkoani Morogoro.
Muonekano wa nje wa soko la kisasa la Manispaa ya Morogoro ambalo ujenzi wake umekamilika.
Msajili wa wahandisi Eng. Patrick Barozi akisisitiza jambo kwa wahandisi wanaosimamia ukarabati mkubwa wa machinjio ya kisasa katika ranch ya
Nguru Hills Mvomero mkoani Morogoro
Muonekano wa machinjio ya kisasa katika ranch ya Nguru Hills Mvomero mkoani Morogoro.
Ujenzi wa mifereji ya kupitisha maji kwenda kwenye mabwawa ya kumwagilia miwa katika shamba la miwa la Mbigiri ukiendelea, shamba hilo ni sehemu ya mashamba yanayomilikiwa na kiwanda cha sukari cha Mkulazi mkoani Morogoro.
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
BODI
ya Usajili wa Wahandisi nchini (ERB), imeridhishwa na kazi za ujenzi wa
miundombinu ya kisasa na kimkakati inayojengwa mkoani Morogoro kwa kuwa
imezingatia viwango vya kihandisi, na ubora unaowiana na thamani ya
fedha.
Msajili wa
Wahandisi Mhandisi Patrick Barozi amesema hayo alipokagua miradi ya
kimkakati ya soko la kisasa la Manispaa ya Morogoro, machinjio ya kisasa
ya Nguru Hills Ranch na miundombinu ya umwagiliaji katika shamba la
miwa la Mbigiri katika kiwanda cha miwa cha Mkulazi.
“Tunawapongeza
wahandisi waliofanyakazi katika miradi hii kwa kuwa wabunifu na
kuzingatia weledi na viapo vyao hali itakayosababisha miradi hii
kukamilika kwa wakati na kutioa fusra za ajira, elimu na biashara kwa
wananchi”, alisema Barozi.
Alisema
ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na wahandisi ni sehemu muhimu ya
majukumu ya ERB lakini pia zoezi hilo ni fusra kwa wahandisi waliopo
katika mafunzo kujifunza na kubadilishana uzoefu na changamoto na
wahandisi walioko kwenye miradi na hivyo kuwajengea uwezo wahandisi
wapya.
Msajili Barozi ametoa wito kwa vyuo vikuu
nchini kuongeza udahili wa wanafunzi katika fani zenye upungufu wa
wataalam ili kuepuka kutumia fedha nyingi kuajiri wataalam kutoka nje ya
nchi.
Naye Msimamizi wa
Ujenzi wa Soko la Manispaa ya Morogoro Mhandisji Juma Gwisu akisema
ujenzi wa soko hilo umekamilika kwa asilimia 99 na kazi inayoendelea ni
kuwapanga wafanyabiashara katika maeneo yao.
"Zaidi
ya wafanyabiashara 2,000 wanatarajiwa kunufaika kwa kufanyabiashara
katika soko hilo la kisasa lililogharimu zaidi ya shilingi bilioni 17,"
alisema.
Kwa upande wake
Meneja wa Ujenzi wa Ranch ya Nguru Hills Mhandisi Grayson Bambanza
amesema machinjio ya ranch hiyo iko katika hatua za mwisho za ukarabati
mkubwa utakaowezesha kuzalisha nyama itakayouzwa katika masoko ya
kimataifa na hivyo kutoa fursa nyingi za ajira kwa wataalam wa mifugo na
kilimo nchini, kuongeza biashara ya kununua mifugo na mazao ya
shambani toka kwa wakulima na wafugaji na hivyo kukuza uchumi wa jamii
mkoani Morogoro.
“Takriban
ng’ombe mia moja na mbuzi na kondoo mia mbili watakuwa wakichinjwa kila
siku katika ranch hiyo itakapokamilika na asilimia 80 ya nyama kuuzwa
nje ya nchi na asilimia 20 pekee ndio itauzwa nchini” amsesisitiza
Mhandisi Bambanza.
Meneja
umwagiliaji wa shamba la miwa la Mbigiri katika Kiwanda cha sukari
Mkulazi Mhandisi Juvenal Matumaini alisema kukamilika kwa mabwawa ya
umwagiliaji katika kiwanda hicho kutawezesha kuanza kwa uzalishaji wa
sukari wa kiwanda hicho kinachotarajiwa kutoa ajira zaidi ya elfu tatu
na mia sita kitakapoanza.
Kiwanda
cha sukari Mkulazi kinachomilikiwa kwa ubia kati ya Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF), na Jeshi la Magereza kiko katika hatua za mwisho kuanza
uzalishaji na kinatarajiwa kuzalisha tani elfu hamsini za sukari kwa
mwaka kitakapoanza kazi na hivyo kuongeza uzalishaji wa sukari nchini na
kutoa fursa nyingi za ajira.
No comments:
Post a Comment