Na Prisca Ulomi, WUUM, Zanzibar
SERIKALI
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
zimeweka saini ya mkataba wa makubaliano wa kuunganisha visiwa vya
Pemba na Unguja na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Mkongo wa Zanzibar
Utiaji
saini huo umeshuhudiwa na katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dkt. Mustafa Aboud Jumbe, Katibu Mkuu
wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar
Utiaji
saini huo umefanywa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano
Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba kwa upande wa Bara na Mhandisi Shukuru
Awadh Slueiman, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Miundombinu ya TEHAMA
Zanzibar (ZICTIA) kwa upande wa Zanzibar
Kabla
ya kushudia tukio hilo, Dk. Zainabu Chaula alisema Serikali ya Muungano
imejenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa gharama ya zaidi ya
shilingi bilioni 700 na kuunganisha kwenye mikoa yote 26 ya Tanzania
Bara na kwenye nchi jirani za Congo, Zambia, Rwanda, Burundi, Kenya,
Uganda na Malawi.
Alisema
maunganisho hayo yanaenda kufungua fursa za wawekezaji na watumia wa
huduma za mawasiliano wa ndani na nje ya nchi kuunganishwa na Zanzibar
kwa kuwa katika kipindi cha miaka mitano tumeshuhudia kuibuka kwa mifumo
ya TEHAMA ambayo inawezesha utoaji wa huduma za mawasiliano kwa
wananchi kwa kasi zaidi
Naye
Dk. Jumbe alisema hayo ndio matunda ya mapinduzi, matunda ya mapinduzi
sio maembe wala mapapai bali ni maendeleo yanayopatikana katika nchi
yetu, na Serikali yetu ya SMZ imetumia zaidi ya shilingi bilioni 30
kuunganisha mikoa na wilaya zote za Unguja na Pemba bali kulikuwa na
changamoto ya kuunganisha Unguja na Pemba ila sasa kwa kupitia
makubaliano haya, tutatumia barabara ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
kuunganisha visiwa Pemba na Unguja na hivyo Zanzibar kuunganishwa na
Tanzania Bara moja kwa moja na utawezesha kupunguza gharama za
mawasiliano ili ziwe nafuu
Mkurugenzi
wa TTCL Kindamba alisema kuwa ufunguzi wa njia za mawasiliano ya Mkongo
kati ya Tanzania Bara na Zanzibar utakuwa na manufaa makubwa sana kwa
taifa hasa katika kuwezesha kuongezeka kwa matumizi ya data na intaneti
na makubaliano hayo yanahusisha kutunza vifaa vya miundombinu ya TEHAMA
vya ZICTIA kwenye majengo ya TTCL
Mhandisi
Suleimani ameongeza kuwa ZICTIA imekamilisha ujenzi wa Mkongo wa
Zanzibar na sasa unaunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambapo
itakuza na kuongeza huduma za mawasiliano; kuondoa changamoto
iliyokuwepo Zanzibar ya kutumia njia ya mawasiliano ya mawimbi ya radio
kutoa huduma za mawasiliano ambayo hayana kasi na ubora unaohitajika,
kupunguza gharama za mawasiliano na kuingizia mapato kwa Serikali.
No comments:
Post a Comment