HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 03, 2020

MSAMA AWAOMBA RADHI TENA WATANZANIA KUAHIRISHWA TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2020

 


TAMASHA la kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania lililokuwa lifanyike Septemba 6 mwaka huu, limeahirishwa kwa mara nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema kuwa kamati ya maandalizi  kushirikiana na maaskofu na wachungaji kutokana na mambo yaliyo nje ya uwezo wao wameona waahirishe tena tamasha hilo.

"Kwa niaba ya wachungaji na maaskofu tumeamua kuhairisha tamasha hilo... Tunaomba mtusamehe mtuvumilie watanzania katika kipindi hiki kigumu kidogo kunamambo ambayo hayajaenda sawa tunajua ni wengi ambao wamekwazika kwahiyo tutapanga tena." Amesema Msama.


Hata hivyo Msama amewaomba radhi  watanzania kwa kuhairisha tamasha la Kuombea uchaguzi Mkuu wa Tanzania Oktoba 28, 2020.

Amesema kuwa tamasha hilo litatangazwa tena siku ambayo itakuwa rafiki kwaajili ya kufanyika ili watu wote waweze kushiriki.


 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijiini Dar es Salaam leo wakati atakingaza kuahirisha Tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania utakaofanyika Oktoba 28, 2020.

No comments:

Post a Comment

Pages