HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 07, 2020

TBS yakamata vipodozi vyenye viambata simu Kariakaoo

NA JANETH JOVIN

SHIRIKA  la Viwango Tanzania (TBS) limefanya ukaguzi wa bidhaa ambazo hazijathibitishwa
katika Soko la Kariakoo na kukutana na baadhi ya vipodozi ambavyo vinatajwa kuwa na viambata sumu.

Akizungumza wakati akiongoza zoezi hilo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa TBS,  Roida Andusamile amesema kuwa katika soko hilo la Kariakoo wamekuta vipodozi venye viambata sumu na haviruhusiwi kuuzwa hapa nchini.

Amesema TBS wataviondoa vipodozi hivyo sokoni na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria kwa kosa hilo la uzaaji wa vipodozi vyenye viambata sumu.

"Tangu Julai mwaka jana, shirika limekuwa likifanya usajili wa bidhaa za vipodozi na vyakula ili kuhakikisha zinapokwenda sokoni au kuhifadhiwa ziwe katika mahali salama na kwamba hakuna madhara yeyote yanayoweza kutokea kutokana na uhifadhi au utumiaji wa bidhaa hizo.

" leo katika soko hilo la Kariakoo tumekuta vipodozi venye viambata sumu na haviruhusiwi kuuzwa hapa nchini, hivyo basi TBS tutaviondoa na wahusika wote watachukuliwa hatua zinazostahili," amesema

Amesema kuwa wahusika hao wamekuwa wakiuza bidhaa hizo kinyemela na sio kwamba hawaelewi utaratibu wanaotakiwa kuufuata wa kusajili bidhaa zao na maeneo wanayohifadhia.

"Watu hawa wamekuwa wakikiuka taratibu hizo na sisi hatuwezi kukaa kimya ndio maana tumekuja hapa kuviondoa ili kuhakikisha soko la Tanzania linakuwa na bidhaa bora na usalama," amesema

Naye Mtathimini na Msajili wa bidhaa za vipodozi kutoka TBS, Ambumi Mwapeta amesema wataziharibu bidhaa zote hizo walizozikamata na kuongeza kuwa anatoa wito Kwa wauzaji wa vipodozi kwenda TBS Kwa ajili ya kuzisaji na kupewa maelekezo mengine ya kitaalam juu ya bidhaa zinazopaswa kuwepo sokoni.

No comments:

Post a Comment

Pages