Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Honest Ngowi, akitoa mada katika mafunzo ya biashara, usafirishaji na ugavi kwa wafanyabiashara ndogondogo (VIBINDO) jijini Dar es Salaam. (Picha na John Dande).
Dk. Musa Maulid, akitoa mada katika mafunzo ya Wajasiriamali wadogo wadogo (VIBINDO)
kuhusu biashara, usafirishaji na ugavi
iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mjasiriamali Aziza Mandari, akichangia mada katika semina ya wajasiriamali wadogo wadogo (VIBINDO) kuhusu biashara, usafirishaji na ugavi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mjasiliamali Mohamed Chitanda,akichangia mada katika semina
ya Wajasiliamali wadogo wadogo (VIBINDO) kuhusu biashara, usafirishaji na ugavi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mradi wa Kuehne Foundation, Dk. Omari Swalehe, akitoa mada katika semina ya wajasiriamli wadogo wadogo (VIBINDO).
Na Mwandishi Wetu
CHUO Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa kushirikina na Kuehne Foundation wametoa mafunzo ya biashara, usafirishaji na ugavi kwa wafanyabiashara ndogondogo (VIBINDO) jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam na Mratibu wa Mradi wa Kuehne Foundatin, Dk. Omary Swalehe amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa wajasiriamali wa biashara ndogo ndogo katika ugavi na usafirishaji wa biashara zao.
"Katika mafunzo haya tumeweza kuwaeleza jinsi wajasiriamali wanavyoweza kufaidika na usafirishaji na Ugavi katika kuboresha biashara zao." alisema Dk. Omary.
Alisema kuwa mafunzo hayo yatawanufaisha wafanyabiashara wadogo wadogo ili kila mmoja atumie mafunzo hayo katika biashara zao.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi akizungumza wakati akitoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo waogo alisema kuwa kila mtu ana ndoto za kuwa mjasiriamali lakini sio wote wanaoweza kufikia malengo yao.
Naye mtoa mada, Dk. Maulid Nzaganza, alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza thamani katika bidhaa ambazo zinathamani ndogo kwa kutumia Teknolojia rahisi.
"Wajasiriamali wadogo wadogo wanaweza kutumia teknolojia kwa mtaji mdogo aliokuwa nao bila ya kuwa na mtaji mkubwa wa kukopa na wenye riba kwa kuuza bidhaa kubwa", alisema Dk. Nzaganza.
"Hapa nimewaonesha bidha iliyokuwa ikiuzwa bei ndogo na baada ya kutumia teknolojia rahisi bidhaa ile ile inaongezeka thamani." Amesema Nzaganza.

No comments:
Post a Comment