Na Lydia Lugakila, Bukoba
Vijana katika Kijiji Cha Kyamalange Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera wameliomba Shirika la Amani mkoani Kagera kuendelea kutoa elimu ya amani na namna ya kupiga kura baada ya vijana hao kukiri kutumiwa katika uvunjifu wa amani katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Vijana hao wameliomba Shirika hilo kuendelea kutoa elimu kwa vijana hao kabla na baada ya uchaguzi ambapo tayari limeanza kuzunguka mkoani Kagera kwa ajili ya kutoa elimu hiyo ya amani na namna ya kupiga kura ambapo vijana waishio katika mwalo wa marehe kata ya Rubafu wamenufaika na elimu hiyo.
Vijana hao wengi wao ujishughulisha na biashara ya na uvuvi wa samaki na Dagaa huku wakidai kuwa husahaulika katika elimu mbambali huku wakilishukuru shirika hilo kuwasogezea huduma hiyo.
Christiani Silvanus na Jamal Ismael Khamis ni vijana walionufaika na elimu hiyo kutoka shirika la amani Mkoani humo wamesema kuwa vijana walio wengi hujikuta wakidanganywa ili kutumika katika uvunjifu wa amani kutokana na kutokuwa na elimu huku baadhi wakisema kuwa chanzo ni uvutaji wa madawa ya kulevya.
Akitoa elimu hiyo ya amani na namna ya kupiga kura Mwenyekiti wa shirika la amani Mkoani Kagera Bwana Maurid Rashid Kambuga amewataka vijana hao kutokubali kutumiwa katika vitendo vya uvunjifu wa amani kwani madhara yake ni makubwa ikiwemo kupoteza Maisha.
Kambuga amesema vijana wanatakiwa kukaa katika misingi ya kutafuta ridhiki huku akiwaomba viongozi wa dini kuihubiri amani kutokana na wao kuwa wadau wa kubwa katika hilo.
Amesema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa kuifuata Sheria utawala Bora kwa maana ya kuongozwa kwa misingi ya katiba ya mwaka 1977 inayotamka usawa wa binadamu na usawa mbele ya Sheria katika ibara 12-13.
Ameongeza kuwa mnamo tarehe 31/3/2018 Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa alitoa wito kwa viongozi wa dini kuhakikisha wanapigania na kulinda amani kwa hali na Mali ikiwa ni pamoja na kipambana na viashiria vya uvunjifu wa amani.
"Vijana msikubali kutumika kwa watu watakaokuja na lugha nzuri na kuwataka mfanye vurugu wao watawadanganya mtalala nje wao na familia zao watalala ndani kwa raha zao huku nyie mkipata mateso wengine kupoteza Maisha msikubali msikubali kutumika"alisema Kambuga.
Aidha amewataka wananchi kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa pale vinapojitokeza vitendo vya u unjifu wa amani.
Kwa upande wake Edwin Bais ambaye ni mwenyekiti wa maafa kutoka shirika la amani amesema shirika hilo limejipanga kuhakikisha linakomesha viashiria vya aina yoyote ya uvunjifu wa amani.
Aidha Bwana Winchislaus Kaidoa ambaye ni afisa uhamasishaji shirika hilo amesema kuwa Tanzania imejaliwa tunu kubwa ya amani ikilinganishwa na nchi nyingine hivyo ni jukumu la Kila Mtanzania kukemea viashiria vya aina yoyote hasa katika kipindi hiki Cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Hata hivyo kwa upande wao viongozi wa dini akiwemo mchungaji wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (T.A.G) Benjamin Emmanuel na Athuman Yahya Koloti wamesema kuwa wamejipanga kuhakikisha kuwa wanaihubiri amani Kila pembe ya nchi.
Winchislaus Kaidoa ambaye ni Afisa Mhamasishaji Shirika la Amani Kagera.
No comments:
Post a Comment