HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 06, 2020

WANAWAKE KKKT USHARIKA WA BOKO WASAIDIA VIFAA TIBA WODI YA WATOTO WENYE SARATANI HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Na Mwandishi Wetu

KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Boko limekabidhi vifaaa mbalimbali vya matibabu kwa Hospitali ya Taifa ya Muhumbili kitengo cha Watoto wenye Ugonjwa wa saratani.

Akikabidhi vifaa hivyo Mchungaji wa Kanisa hilo, Ambakisye Lusekelo, amesema wamekabidhi vifaa ambavyo vitatoa msaada wa kimatibabu kama ambavyo Ungozi wa Muhimbili ulitoa Muongozo huku akiwatakia heri na amani katika huduma wanazozipata.

"Tupo kwa ajili ya matendo ya huruma ya kusaidiana, tunaomba Mungu sana aendelee kuwanganga na kuwaponya lakini awatie nguvu na kuwatia moyo na kuwapa amani wazazi na walezi ambao wanawahudumia, Madakatari wetu pia tunawakabidhi mikononi mwa Mungu azidi kuwapa upendo kwa watoto hawa.

"Damu ya Yesu ikiambatana na vifaa hivi tulivyovileta itakwenda kuwaponya hawa watoto, kufika kwetu hapa ni kwa ajili ya nguvu na uweza wa Mungu mwenyewe kwamba kwa njia ya matendo ya huruma, Yesu akawakumbuke watoto wetu Ameen."amesema Lusekelo

Baadhi ya wakinamama wa Umoja wa Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 katika wodi ya watoto ya wagonjwa wa  saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mwenyekiti wa Kwaya ya Umoja wa Wanawake Kanisa la KKKT Usharika wa Boko, Mama Lema (kushoto) na Mama Milen wakielekea katika Wodi ya Upendo kukabidha vifaa tiba.
Baadhi ya walezi na wazazi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na akinamama wa Umoja Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko
Maelekezo.

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko, Ambakisye  Lusekelo, akiongoza maombi kabla ya kukabidhi vifaa tiba.
Mzee wa Kanisa Ruth Mloge, akisoma neno la Mungu.
Katibu Msaidizi Umoja wa Wanawake KKKT Usharika wa Boko, Prisca Ndambala, akisoma neno la Mungu.
Mwenyekiti wa Kwaya ya Umoja wa Wanawake KKKT Usharika wa Boko, Mary Lema, akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa tiba.
Mweka Hazina wa Msaidizi wa Umoja wa Wanawake wa KKKT-Boko, Magdalena Nyellah, akifafanua jambo wakati wa kukabidhi vifaa tiba katika Wodi ya Upendo na Tumaini
Muuguzi katika wodi ya Tumaini, Asteria Henjewele, akizungumza wakati wa kupokea vifaa tiba kutoka kwa kikundi cha Umoja wa Wanawake wa Kanisa la KKKT Usharika wa Boko jijini Dar es Salaam.
Kukabidhi chandarua.

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Boko, Ambakisye  Lusekelo, akikabidhi sehemu ya msaada wa vifaa tiba kwa wauguzi wa wodi ya Watoto wanaougua saratani katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

No comments:

Post a Comment

Pages