Mgombea ubunge Jimbo la Bukoba mkoani Kagera, Dokta Samson Rweikiza, akiwahutubia wananchi katika kampeni zake.
Na Lydia Lugakila, Bukoba
Mgombea ubunge Jimbo la Bukoba vijiji ni mkoani Kagera kupitia CCM Dk. Jasson Rweikiza ameahidi kuanzisha kituo cha maendeleo ya vijana wanaomaliza darasa la saba na wanachuo wanaokaa kijijini bila kuwa na uwezo wa kujiunganisha ili waweze kupata stadi za kuandika andiko za miradi zitakazowasaidia kwenda benki na kuomba mikopo.
Dk. Rweikiza ametoa ahadi hiyo katika uzinduzi wa kampeini za chama hicho zilizofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nyakaju Kata ya Rubare Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.
Rweikiza amesema kuwa tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani 2015 elimu nchi nzima imekuwa bure ambapo wilaya ya Bukoba vijijini imenufaika na mpango huo ambapo vijana wengi ambao walikuwa hawaendi shule kwa kukosa ada na michango sasa wanaenda shule na elimu inazidi kuboreshwa ambapo shule 6 za msingi zinajengwa wilayani humo.
Rweikiza amesema kuwa endapo atachaguliwa tena kuongoza jimbo hilo kutokana na ilani yake binafsi atahakikisha anaokoa jahazi la vijana waliomaliza darasa la saba na wanavyuo vikuu waliokaa vijijini baada ya kumaliza elimu hiyo bila kuendelezwa.
Amesema kuwa kituo hicho cha maendeleo ya vijana yatasaidia vijana hao kujiunga katika makundi na kupata mikopo, kufanyabiashara , kupata ajira na kujiajiri na kuajiriwa ambapo watapata uwezo wa kuunganishwa na kupata stadi za kuandika andiko za miradi kazi ambayo ameahidi kuanzisha.
No comments:
Post a Comment