Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Singida, Alex Mkumbo, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Ni furaha tupu wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,akinunua moja ya kitabu hicho kwa sh.milioni moja.
Burudani ikitolewa kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ameanza kazi kwa kishindo katika kipindi chake cha awamu ya pili kwa kuzindua kitabu na kufanikisha kununuliwa kwa thamani ya sh.milioni 28.
Kitabu hicho kinachoitwa Misemo na Methali za Wanyaturu kilichoandikwa na Mchungaji Dkt.Syprian Yohana Hilinti (PhD) kilizinduliwa jana katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Singida mjini na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi huku mshereheshaji wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho akiwa ni Mbunge wa Iramba, Mwigulu Nchemba.
Katika uzinduzi huo Mtaturu ambaye alikuwa mgeni rasmi alinunua kitabu kimoja kwa sh.milioni moja jambo lililoongeza ari ya watu waliokuwepo kwenye hafla hiyo kujitokeza na kununua vitabu hivyo kwa fedha taslimu.
Katika hatua nyingine Mtaturu alinunua pikipiki sita kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kanisa hilo mkoani humo ambapo pia Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba alichangia pikipiki tatu jumla zikiwa tisa.
Askofu wa kanisa hilo Mkoa wa Singida, Alex Mkumbo aliwashukuru wabunge hao kwa msaada huo.
No comments:
Post a Comment