HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 19, 2020

TAMWA ZANZIBAR WAWATAKA WAJASIRIAMALI KUONGEZA UFANISI KATIKA UZALISHAJI BIDHAA

Afisa uwezeshaji kiuchumim TAMWA-Zanzibar, Nairat Abdalla Ali, akionesha mfano wa bidhaa ambazo zimethanifiwa vyema katika mfumo mzima wa vifungashio kwa wajasiriamali.
Afisa Masoko kutoka TAMWA-Zanzibar Muhidini Ramadhani akisisitiza jambo kwa wajasiriamali juu ya umuhimu wa kutokata tamaa na kuzalisha bidhaa bora zaidi.

 

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

 

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-Zanzibar kimewataka wajasiriamali wanaowasimamia kuhakikisha wanaongeza ufanisi katika uzalishaji wa bidhaa ili ziweze kuwa kivutio kwa lengo la kuongeza kipato  kwa manufaa yao.

 

Akizungumza na wajasiriamali hao Afisa uwezeshaji uchumi Nairat Abdalla Ali katika ukumbi wa Chama hicho uliopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja   aliwataka  wajasiriamali hao kutumia fursa wanazopatiwa kila siku zikiwemo za kujengewa uwezo kuwa sehemu ya mabadiliko.

 

Alisema  kikawaida  ili mteja anunue bidhaa anahitaji kuona ubora wa bidhaa hizo na sio kuzalisha bidhaa zisizokua na kiwango ambazo anaamini haziwezi kufanya vizuri sokoni.

 

Awali afisa masoko kutoka Tamwa-Zanzibar Muhidini Ramadhan aliwataka wajasiriamali hao kutokata tamaa na changamoto zinazowakabili.


Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto mbali mbali wakati wa uzalishaji wa bidhara hizo lakini hawapaswi kuzichukua chanagamoto hizo kuwa sababu ya kukata tamaa na kuacha kuzalisha.

 

‘Sisi TAMWA tunfaham muna chanagmoto nyingi zinazowakabili lakini nawaomba msikate tamaa na zigeuzeni changamoto hizo kuwan sehemu ya fursa’aliongezea.

 

Aidha Afisa huyo wakati akiendelea kufafanua zaidi alisekma miongoni mwa njia kuu ambazo zitawafanyia wajasiriamali hao kupiga hatua zaidi ni kujenga mashirikiano baina yao na wadau wengien mbali mbali ambao wanaamini watakaua miongoni mwa nyezo za kukuza fursa zaidi ikiwemo kupata masoko.

 

Kwa nyakati tofauti baadhi ya wajasiriamali hao walisema miongoni mwa changamoto wanazokutana nazo ni upatikanaji wa vifungashio vya bidhaa zao mara wanapomaliza kuzalisha.

 

Mmoja miongoni mwao Faida Mohamed Shaibu  alisema ni pamoja na uhaba wa masoko ya uuzaji wa bidhaa hizo lakini uhaba wa vifungashio imekua tatizo kubwa kwao.

 

Alisema mara nyingi wamewahi kuzalisha bidhaa lakini hukosa kabisa vifungashio ambavyo huhitajika katika utunzaji wa bidhaa hizo kwa mfano chupa na nyenginezo na huelezwa kuwa mzigo haujafika.

 

‘Kutokana na mazingira ya aina hii wakati mwengine tunalazimika kubaki na bidhaa zetu majumbani bila ya kuwa na saehemu sahihi ya kuhifadhi na kupelekea kuharibika’ aliongezea.

 

Huku hayo yakijiri alizomba taasisi mbali mbali za kiserekali na watu binafsi kuwekeza nguvu zao katika uzalishaji wa bidhaa za ndani kwa lengo la kuwainua wajasiriamali wa Zanzibar ili waweze kupiga hatua zaidi za kimaendelea na kuliongezea pato taifa kupitia sekta ya kodi.

No comments:

Post a Comment

Pages