HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 19, 2020

TOTAL YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUWATHAMINI ZAIDI WATEJA WAKE


Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Bw. Jean-Francois Schoepp, akizungumza katika hafla ya kuzindua wiki ya huduma kwa wateja ya Total kwa mwaka huu wa 2020, katika kituo cha mafuta cha Total Africana, kilichopo êneo la Africana, Mbezi Beach, Dar es Salaam. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Kwa Total, mteja ni zaidi ya mteja, ni mshirika”. Maadhimisho hayo yanaadhinishwa kwa wiki nzimakwa shughuli mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Bw. Jean-Francois Schoepp, akionyesha unaweza kulipia huduma kwa kadi yako ya benki wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ya Total kwa mwaka huu wa 2020, katika kituo cha mafuta cha Total Africana, kilichopo êneo la Africana, Mbezi Beach, Dar es Salaam. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Kwa Total, mteja ni zaidi ya mteja, ni mshirika”. Maadhimisho hayo yanaadhinishwa kwa wiki nzima kwa shughulimbalimbali.
Wakati wa wiki ya wateja wa Total, hakuna bosi kukaa ofisini, wote ni kuhudumia wateja, Mkurugenzi wa sheria na mahusiano wa Total, Tanzania, Bi. Marsha Msuya Kileo, akisafisha kioo cha gari ya mteja, wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ya Total kwa mwaka huu wa 2020, katika kituo cha mafuta cha Total Africana, kilichopo êneo la Africana, Mbezi Beach, Dar es Salaam. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Kwa Total, mteja ni zaidi ya mteja, ni mshirika”. Maadhimisho hayo yanaadhinishwa kwa wiki nzima kwa shughuli mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Bw. Jean-Francois Schoepp, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa sheria na mahusiano wa Total, Tanzania, Bi. Marsha Msuya Kileo, wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ya Total kwa mwaka huu wa 2020, katika kituo cha mafuta cha Total Africana, kilichopo êneo la Africana, Mbezi Beach, Dar es Salaam. 

Wafanyakazi wa Total Tanzania, katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Bw. Jean-Francois Schoepp, (katikati mwenye kofia nyekundu) wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ya Total kwa mwaka huu wa 2020, katika kituo cha mafuta cha Total Africana, kilichopo êneo la Africana, Mbezi Beach, Dar es Salaam.
 


 Na Mwandishi Wetu

 

Kampuni ya mafuta ya Total, ambayo ndio kampuni inayoongoza kwenye uuzaji na usambazaji wa mafuta nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 50, imezindua wiki ya huduma kwa wateja kwa kuwathamini zaidi wateja wake kuwa ni zaidi ya wateja, sasa ni washirika wa Total.
 

Akizungumza katika hafla ya kuzindua wiki ya huduma kwa wateja ya Total, Mkurugenzi Mkuu wa Total Tanzania Bw. Jean-Francois Schoepp alisema, “Total tunaamini na kutambua kuwa wateja wetu ni zaidi ya wateja, ni washirika wetu. Wao ndio chanzo cha biashara na mafanikio ya Total
nchini.

 Tunawashukuru sana kwa kuendelea kutuunga mkono na kutuamini. Tunawakaribisha wote kutupa mawazo na maoni yenu juu ya huduma zetu ili tupate kuziboresha na kuwapa huduma bora zaidi.”


Aidha aliongeza kuwa, Total imekuwa ya mafanikio makubwa sana kutokana na jitihada za wafanyakazi wa Total na kuwashukuru wafanyakazi wa Total kwa kujituma katika kuhakikisha kuwa Total imekuwa ya mafanikio.


Kwa upande wake, Mkufunzi wa Vituo vya Total, Msafiri Josephat Shigella, amesema lengo la maadhimishoya wiki ya mteja ni kutoa fursa kwa uongozi na menejmenti ya Total, kukutana ana kwa ana na wateja, kuwasikiliza na kujua mahitaji yao.
 

Mkurugenzi wa Mtandao wa vituo vya mafuta vya Total, Marriame Saw, amewashukuru sana wateja wa Total kwa kuichagua Total na kuahidi kuendelea kupanua mtandao wa vituo vya mafuta vya Total ambayo kwa sasa, tayari wanavyo vituo zaidi ya 100.


Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Total. Marsha Msuya Kileo, ameendelea kuwasisitiza watumia wa mafuta, waendelee kutumia mafuta ya Total,yenye kiambata cha excellium, ili kufaidi mafuta na vilaini na huduma zenye ubora wa hali ya juu.


Kwa upande wa wateja, wateja waliohojiwa, wamesema mafuta ya vituo vya Total yana tofauti fulani na mafuta mengine yote, ila pia vituo vya Total, vina muonekano fulani unaokufanya wewe dereva kujisikia vizuri kujaza mafuta Total, pia unahudumiwa vizuri.

No comments:

Post a Comment

Pages