HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 19, 2020

Waandishi wa habari watakiwa kuilinda taaluma yao, kuwa chachu ya maendeleo

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi amewataka wanahabari kuilinda taaluma yao na kutekeleza wajibu wao kwa kulinda amani ya nchi na kuwa chachu ya maendeleo.

Abbasi ameyasema hayo leo  wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari Nchini (UTPC) uliofanyika kwenye Hoteli ya Flomi mkoani Morogoro.

Akifungua mkutano huo, Dkt. Abbasi amesema Serikali ya Awamu ya Tano katika muhula huu wa Pili tayari Rais Dkt John  Magufuli ameahidi kuendelea kuimarisha mazingira yao ya kufanyakazi.

Aidha Dk. Abbasi amewataka waandishi wa habari  wajenge hoja juu ya mambo gani mahsusi wanayoona Serikali inapaswa iyasimamie zaidi kwa maslahi yao badala ya kupiga kelele tu.

"Pia niwakumbushe tu wale ambao itafika Desemba Mosi, 2021 wanasoma diploma ya uandishi  hawajamaliza wataendelea na kazi ila wale ambao watakuwa bado hawajaanza basi ndio mwisho," amesema  Dk. Hassan Abbasi.

No comments:

Post a Comment

Pages