HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 21, 2020

Equity Tanzania yazindua nembo mpya


Nembo mpya sasa kuonyesha “Equity” bila neno Benki kama ilivyozoeleka ili kuonyesha dhamira ya kampuni ya kuwa kituo cha kutoa huduma mbali mbali jumuishi zakifedha ndani ya paa moja. 


Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Mhandisi Raymond Mbilinyi, wakizindua nembo yao mpya ya Equity Tanzania katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania Robert Kiboti (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Mhandisi Raymond Mbilinyi, wakipongezana mara baada ya kuzindua nembo yao mpya ya Equity Tanzania.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Equity Tanzania, Ester Kitoka, akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
Muonekano wa nembo mpya na ile ya zamani.


Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa nembo yao mpya inayoendana na safari ya mabadiliko.


Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Tanzania Mhandisi Raymond Mbilinyi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo yao mpya. 


Mkurugenzi Mwendeshaji wa Equity Tanzania, Ester Kitoka, akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari wakati wa hafla hiyo. 

Mjumbe wa Bodi ya Eguity, Prof. Honest Ngowi, akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa Benki ya Equity.


Dar es Salaam, Tanzania  

Equity Tanzania leo imezindua utambuzi mpya unaoendana na safari ya mabadiliko inayoendelea ndani ya kampuni mama ya Equity Group Holdings.

Utambuzi huo mpya unalenga kuiweka kampuni katika njia ya ukuaji endelevu na utoaji huduma bora zinazoendana na mabadiliko yanaoendelea katika mazingira ya sekta ya fedha.

Kuanzia sasa, Equity Tanzania itajitambulisha kwa nembo iliyobeba kikapu kilichosheheni bidhaa na huduma mbali mbali zakifedha chini ya paa moja.

Nembo mpya sasa kuonyesha “Equity” bila neno Benki kama ilivyozoeleka ili kuonyesha dhamira ya kampuni ya kuwa kituo cha kutoa huduma mbali mbali jumuishi zakifedha ndani ya paa moja.

Akizungumza kuhusu uzinduzi wa nembo mpya, Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Tanzania, Robert Kiboti alisema muonekano huo unaambatana na ahadi ya usimamizi imara wa uhusiano, uwezeshaji wa wateja binafsi na biashara.

“Muonekano wetu mpya unaleta uhakika wa uwezeshaji wa watu binafsi ili kupanua fursa zao katika kuleta utajiri. Tutazindua muonekano mpya katika matawi yetu yote, njia zetu za kutolea huduma zakibenki kidijitali, mitandao yakijamii, tovuti, njia zakibenki kupitia simu za kiganjani, biashara mtandaoni na mashine za kutolea fedha. Kuanzia sasa mtaanza kuona alama za nembo yetu mpya katika matawi yetu ikiwa ni sehemu ya programu yetu ya mabadiliko,” alisema Kiboti.

Wateja watarajie kupata huduma bora kabisa bila kuwepo na aina yeyote ya hitilafu wakati benki ikijipanga kukuza idadi ya wateja wake.

“Tutaendela kubuni huduma bora kwa lengo la kupanua upatikanaji wa huduma jumuishi zakifedha nchini kote…Tutaimarisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa njia ya simu za kiganjani na kupeleka huduma zetu mpaka maili ya mwisho kupitia Equity Wakala. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa Mawakala wetu wanaendelea kujipatia pato la ziada na kutengeneza ajira mijini na vijijini. Tunaahidi kuendelea kuwa wabunifu na wenye umuhimu wakati ambapo mahitaji ya wateja wetu yanabadilika kulingana na malengo na ndoto zao,” alisema Kiboti.  

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Equity Group Holdings Plc, Dk James Mwangi alisema: “Mazingira ya biashara yamebadilika kutokana na mabadiliko ya mahitaji na matamanio ya wateja yanavyokwenda sambamba na mabadiliko ya mtindo wa maisha ya wateja ambayo [mabadiliko] yameletwa na maendeleo ya teknolojia. Vile vile, mahitaji ya soko hivi sasa yanatubidi kuwa na bidhaa na huduma zinazopendwa na vijana pamoja na kwenda zaidi kijiditali. Wateja wengi siku hizi hupendelea zaidi kujihudumia badala ya kwenda benki. Equity itaendelea kubuni huduma zake ili kuendana na mahitaji ya wateja ya sasa na ya baadaye”.

“Muonekano wetu mpya unaonyesha dira ya kule tunakotaka kwenda. Ni muonekano unaowasilisha uwezo wetu ulivyo mkubwa duniani, urithi wetu wenye nguvu, utamaduni wetu wa ubunifu na mtindo wa biashara ulio bora utakaobeba chapa yetu na kuipeleka popote pale barani Africa na duniani kote,” alisema Dk Mwangi.

Mabadiliko makubwa katika mwelekeo wa chapa hii mpya ni kuzindua neno unganishi la Equity MOJA.  

Kwa muonekano wa nembo, kutakuwa na neno “Equity” tu bila neno nyingine lolote la biashara zake kama ilivyozoeleka kama vile Benki, Bima, Benki ya Uwekezaji na mengineyo.

Kwa muktadha huo, Equity sasa itajitangaza duniani kote kama kikapu kimoja chenye huduma na bidhaa mbalimbali za kifedha chini ya paa moja zikiwemo zakibenki, za bima na za uwekezaji.

Benki itaendelea kuwekeza na kufanya kazi kwa faida ya nchi ikiwa ni pamoja na elimu ya maswala ya fedha na upatikanaji wake, ujasiriamali, kilimo, ubunifu na mazingira.

Uzinduzi wa utambuzi mpya wa Equity Group Holdings ulianzia nchini Kenya. Kwa sababu hiyo, Equity South Sudan, Equity Uganda na Equity Tanzania nazo zinatarajia kuzindua utambuzi huo mpya.

No comments:

Post a Comment

Pages