HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 18, 2020

CMA KUTOA UAMUZI WA GREENWASTE PRO DESEMBA 21, 2020

 Mwandishi Wetu

Baraza la Usuluhishi na Uamuzi (CMA) imehairisha kutoa uamuzi mdogo wa mgogoro wa waliokua wafanyakazi wa Kampuni ya kuzoa taka Jiji la Dar as Salaam, GreenWaste Pro Limited dhidi ya mwajiri wao.

Kutokana na hali hiyo, uamuzi huo utatolewa Desemba 21 Mwaka huu baada ya kukamilika kuandikwa kwa hukumu.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya wafanyakazi hao na mwakilishi wa kampuni hiyo, Msuluhishi wa mgogoro huo, Mpulla alidai kuwa, kutokana na mwingiliano wa majukumu, uamuzi huo utatolewa Desemba 21 mwaka huu.

Wafanyakazi hao walikimbilia katika baraza hilo kwa madai ya kuachishwa kazi kinyume na taratibu za kisheria na mikataba yao ya kazi hali iliyosababisha kuishi katika mazingira magumu.

Shauri la wafanyakazi hao lilisikilizwa leo katika Baraza hilo chini ya msuluhishi Mpulla ambapo wafanyakazi 13 waliokua wakifanya kazi katika kampuni hiyo wamedai kuwa, kampuni iliwaondoa kazini bila ya kufuata utaratibu wa kisheria.

Walidai kuwa Februari 12,2020 kampuni hiyo iliwakamata wafanyakazi hao ambao ni 13, na kuwapeleka polisi kwa madai ya wizi wa fedha za kampuni huku akisitisha mikataba ya ajira bila ya kufuata utaratibu wa kisheria.

Walidài kuwa wakati wanakamatwa walikua hawajapewa taarifa yoyote ya kuonyesha wameachishwa kazi.

Walidai kuwa upelelezi wa shauri hilo ulichelewa hali iliyosababisha kushindwa kuwasilisha shauri hilo kwenye baraza hilo kwa wakati.

Aliiomba baraza hilo kusikiliza madai yao na kuyatolea uamuzi ili haki itendeke kutokana na kutolipwa haki zao katika kipindi chote walichokua wanafanyakazi.

Hata hivyo, Wakili wa Kampuni ya GreenWaste Pro Limited, Evans Ignas alidai kuwa hoja zilizowasilishwa na wafanyakazi hao ni batili kwa madai kuwa wanaweza kufungua shauri kwenye baraza hilo hata kama upelelezi unaendelea.

Alidai kuwa, wafanyakazi hao waliondolewa kazini kwa kufuata taratibu za kisheria na kwamba hakuna aliyeondolewa kinyume na kuliomba baraza hilo kutupilia mbali madai hayo.

No comments:

Post a Comment

Pages