Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato akimsikiliza Msimamizi wa Kituo
cha Kupoza Umeme Kibeta Ndg. Samson Kuboja, wakati alipofika Kituoni
hapo kufahamu utendaji kazi wake.
Serikali kupitia Wizara ya Nishati inaendelea kuboresha Huduma ya Umeme kwa kununua mitambo mipya zikiwemo Transfoma, pamoja na kusimamia Ujenzi wa Miradi ya Kufua Umeme ya Rusumo na Kikagati, ili kuondokana na adha ya kukatika kwa Umeme Mkoani Kagera, sambamba na kuachana na Umeme wa kununua kutoka Nchi Jirani ya Uganda.
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Nishati Adv. Stephen Byabato wakati wa
ziara take ya kutembelea na Kukagua Vituo viwili Vya kupoza na
kusambaza Umeme Vilivyopo Kibeta Manispaa ya Bukoba, na Kyaka Wilayani
Missenyi Mkoani Kagera na Kuridhishwa na Utendaji kazi wa Vituo hivyo,
mapema Desemba 23, 2020.
Akiwa
katika Kituo cha kupoza umeme Kibeta, Naibu Waziri wa Nishati
ameshuhudia Mitambo mipya na Kisasa iliyojengwa eneo hilo, yenye uwezo
wa kuzalisha na kusambaza Umeme wa kiasi cha Megawati 16 huku matumizi
ya Umeme kwa Wananchi wa Mkoa Kagera kwa Ujumla Ni Megawati 10.2 mpaka
12 kwa Sasa.
Naibu Waziri
Byabato amenukuliwa akisema "..Nimeridhishwa na Utendaji wa Kituo hiki
Cha Kupoza Umeme, kazi yao Ni Nzuri ndio maana tunapata Umeme wa
Uhakika, ukiacha changamoto ndogo ndogo ambazo, husababishwa na Mambo
mbalimbali ikiwemo Hali ya hewa." Amesema Byabato.
Aidha
Naibu Waziri wa Nishati Adv. Stephen Byabato ameishukuru Serikali kwa
namna ambavyo imeboresha Miundo mbinu madhubuti na ya Kisasa, ambayo
imekuwa na mchango Mkubwa wa kuinua Uchumi wa Mkoa Kagera kupitia
Viwanda na mengineyo. Mhe. Byabato ameongeza kuwa kwa Sasa Serikali
kupitia Wizara ya Nishati, ipo katika Mpango wa kununua Transfoma
nyingine mbili kubwa zitakazokuwa na uwezo wa kuzalisha Umeme Megawati
60 kila moja, lengo likiwa Ni kwendana na kasi ya Tanzania ya Viwanda,
tunapoingia Uchumi wa Kati.
Naibu
Waziri Byabato ameendelea kuwasihi Wananchi kulinda na kutunza Miundo
mbinu ya Umeme, kwa Kuzingatia umuhimu wa Nishati hiyo kwa Matumizi ya
kila siku, pamoja na kutojaribu kuhujumu Vifaa na Miundo mbinu ya
Kuzalisha Umeme kwa kile kinachoitwa kuuza vyuma chakavu, Jambo ambalo
husababisha hasara kubwa kwa Taifa.
Wakati
huohuo Naibu Waziri Byabato, ametembelea kituo cha kupoza Umeme cha
Kyaka, ambacho hupokea Umeme huo kutokea Uganda na kuridhishwa na
Utendaji Kazi, na baadae akapata nafasi ya Kusikiliza Wananchi
waliojitokeza kuwasilisha Kero zao sugu, ambazo Baadhi zilipatiwa majibu
palepale na nyingine zikiendelea kutatuliwa.
Hayo
yanajiri wakati jitihada za Ujenzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Rusumo -
Ngara, wa Megawati 80 na ule wa Kikagati - Kyerwa Megawati 14
zikiendelea ili kuhakikisha Mkoa Kagera unapata Umeme wake na
kuunganishwa katika Gridi ya Taifa, ili kuondokana na Matumizi ya Umeme
kutoka Uganda kama ilivyo Sasa, ambapo Serikali imekuwa ikitumia pesa
Nyingi kununua Umeme huo kutoka Nchi Jirani.
No comments:
Post a Comment