HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 24, 2020

Milioni 400 kutoka COSTECH zatumika kujenga Maabara ya Kudhibiti Ubora wa Chakula


 

Mkurugenzi wa mradi Dkt. Purificator Kiwango akieleza namna mradi unavyotekelezwa.


 Mtafiti akionesha namna wanavyopima sampuli  mbalimbali katika maabara hiyo. 


 

NA MWANDISHI WETU

 

SERIKALI kupitia Tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetoa kiasi cha Sh.Milioni 400 kwa Shirika la Utafiti wa Viwanda na Maendeleo Tanzania (TIRDO) ili kukabiliana na upungufu wa vifaa vya maabara.

 

TIRDO ambayo ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 5 ya mwaka 1979, na kuanzisha maabara ili kusaidia sekta ya viwanda ya Tanzania kwa kutoa utaalamu wa kiufundi na huduma za kuboresha msingi wa teknolojia pamoja na utafiti kwenye viwanda.

Shirika hilo liliomba na kupatiwa ruzuku ya kiasi cha Sh. Milioni 400 kutoka Serikalini kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ili liweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.,

 

Akizungumzia kuhusu TIRDO,Mtafiti Kiongozi wa mradi huo, Dkt.  Purificator, Kiwango anasema mpaka sasa kuna jumla ya wanafunzi watafiti 47 ambao ni wanufaika katika mazao ya kilimo.

 

Anasema TIRDO imekuwa ikikabiliana na changamoto ya upungufu wa vifaa vya maabara vinavyotumiwa na watafiti-wanafunzi pamoja na wajasiriamali wanaosindika na kusafirisha mazao ya chakula ndani na nje ya nchi hivyo kushindwa kuthibitisha ubora wa mazao na bidhaa zitokanazo na kilimo.,

Anasema ruzuku hiyo imesaidia ununuzi wa vifaa muhimu vya kuwezesha upimaji wa sumu kuvu, kiwango cha madini katika chakula, kiwango cha viini lishe.

 

“Maboresho ya miundombinu ya maabara hiyo yamewezesha kuanza kufanya kazi kwa kupima sampuli mbalimbali za mazao yatokanayo na kilimo kwa kuwanufaisha Watanzania na wataalamu wa TIRDO ambao wameongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao”anasema Dkt.Kiwango

 

 

Kwa upande wake Grace Laizer ambaye anamiliki kiwanda kinachotengeneza siagi ya karanga (Peanut Butter) anasema yeye amekuwa akipima sampuli za karanga anazozizalisha katika maabara hiyo.

“Maabara hii ina mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa kwa kuwa imeimarisha udhibiti ubora wa vyakula kwa viwango vya kitaifa na kimataifa”Anasema Laizer



No comments:

Post a Comment

Pages