HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 20, 2021

ASKARI POLISI AJINYONGA HADI KUFA-KIBAHA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na tukio hilo.


Aliyekuwa askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani mwenye  namba E 6472  marehemu Yusuph Said (52), ambaye alijinyonga katika  nyumba yake aliyokuwa anaijenga katika maeneo ya Kata ya Kongowe akiwa katika picha na wenzake enzi za uhai wake. (Picha na Maktaba). 

  

 

NA VICTOR MASANGU, PWANI 

 

ASKARI wa Jeshi la   Polisi aliyekuwa anafanyakazi katika Kituo cha Polisi wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani  namba E 6472   Yusuph Said  mwenye umri wa miaka (52)  amekutwa  amejinyonga hadi kufariki dunia  katika  nyumba yake anayoijenga katika maeneo ya miembe saba   kata ya Kongowe wilaya ya Kibaha.

 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea katika eneo la Miembe saba B  kata ya Kongowe wilayani Kibaha ambapo alisema tukio hilo lilitokea Januari 18 majira ya saa 12 jioni.

 

Kamanda Wankyo alisema Yusuph alikua akitumikia katika kituo c anaishi Picha ya Ndege lakini siku ya tukio alienda Kongowe eneo ambalo anaendelea na ujenzi na ndipo alipokutwa amejinyonga na kamba.

 

Kamanda alibainisha kwamba uchunguzi kuhusiana na tukio hilo unaendelea wakati taratibu za kumsafirisha marehemu kwenda kwao Lindi kwa maziko zikiendelea.

 

Msaidizi wa balozi kwenye eneo hilo Imelda Kitosi alisema akiwa nyumbani alipigiwa simu kuwa kuna tukio la mtu kujinyonga ndipo akaenda kushuhudia akiwa na baadhi ya majirani.

 

Imelda alisema alipofika alielezwa na wazazi wa watoto waliokuwa karibu ya eneo hilo kuwa kuna watoto waliokuwa wanacheza kombolela nje ya nyumba hiyo ambao walisema walisikia mtu anajipiga ndani ya nyumba na walipochungulia wakamkuta tayari yupo chini akiwa na kamba shingoni na walikimbia kwenda kutoa taarifa.

 

Wazazi hao walipofika katika nyumba hiyo ambayo bado inajengwa walimkuta askari huyo tayari ameshafariki ndipo walipoanza kutoa taarifa kwa viongozi na kumpigia msaidizi huyo wa balozi.

 

"Mimi sasa baada ya kupigiwa simu niliingia hapa pamoja na baadhi ya watu waliokuwa karibu tulimkuta yuko kwenye chumba ambacho kilikua kinajengwa kama bafu au choo kamba kaifunga juu na chini kulikua na tofali ambalo baada ya kuhangaika sana mguu mmoja tulikuta kama umepiga goti na mwingine umeegemea tofali huku kamba ikiwa shingoni" alisema.

 

Balozi huyo alieleza kuwa baada ya kushuhudia tukio hilo ndipo walipiga simu Polisi kutoa taarifa na walifika na kuchukua mwili wa marehemu.

No comments:

Post a Comment

Pages