WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Njisia,Wazee na Watoto Dkt. Dorothy
Gwajima.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Njisia,Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema Tanzania kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wapya wa Saratani wapatao 50,000.
Nainakadiriwa kuwa, ifikapo mwaka 2030 kutakuwa na ongezeko la asilimia 50 ya wagonjwa wapya wa saratani.
Hayo
yameelezwa leo na Waziri huyo wakati wa uzinduzi wa idara ya magonjwa
ya saratani,huduma za patholojia na mkataba wa mteja kwenye hospitali
ya Benjamin mkapa
Dkt.
Gwajima amesema kuwa ongezeko hilo kwa mujibu wa Takwimu za Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Tafiti za Saratani (IARC) na
kuongeza kuwa Takwimu za hapa nchini za 2018 zinaonyesha kuwa idadi ya
wagonjwa wapya wa Saratani ni 14,028 sawa na asilimia 33.3 ya wagonjwa
wote nchini.
“Saratani
kama moja ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza inashika nafasi ya tano kwa
wanaume na ya pili kwa wanawake kwa kusababisha vifo vitokanavyo na
magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchini.
Kwa
ujumla Saratani zinazoongoza kwa wanawake ni mlango wa kizazi na
Saratani ya Matiti. Kwa wanaume, Saratani zinazoongoza ni Saratani za
Tezi Dume, Koo pamoja na Kichwa na Shingo.
Aidha,
Dkt. Gwajima amesema Magonjwa ya Saratani yanatibika iwapo tu mgonjwa
atawahi kupata tiba katika Vituo vya Afya vinavyotoa huduma hiyo. Zaidi
ya asilimia 75 ya wagonjwa wa Saratani hufika katika Vituo vya Matibabu
wakiwa wamechelewa sana na kuwawia vigumu madaktari kutibu na kuponya
ugonjwa huo.
“Nitoe rai
kwa wananchi, tujenge tabia ya kupima afya zetu mara kwa mara ili
ikibainika kuwa tuna changamoto za kiafya basi tuanze matibabu bila
kuchelewa”Alisisitiza Dkt. Gwajima
Aidha,
amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau na mashirika yasiyo ya
Kiserikali imeendelea kuhakikisha inapambana na magonjwa ya saratani,
ambapo katika kukabiliana na hilo Serikali imefunga mashine mbili za
kisasa za tiba ya saratani kwa njia ya mionzi aina ya LINAC katika
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ambazo zimeanza kutoa huduma tangu
Septemba, 2018.
Dkt.
Gwajima aliongeza kuwa Serikali imeanzisha vituo takribani 624 ambavyo
huweza kugundua na kutibu mapema saratani ya mlango wa kizazi.
Hata
hivyo Dkt. Gwajima alifurahishwa na wataalamu wazawa wa Hospitali ya
Benjamin Mkapa na wale wa Chuo Kikuu Dodoma kwa kujituma, kuwajibika na
kuthubutu kuanzisha na kutoa huduma za kibobezi katika upandikizaji wa
Figo.
“wagonjwa 16
wamepandikizwa Figo ndani ya kipindi cha miaka mitatu, kati yao wagonjwa
5 wamepandikizwa na wataalamu wetu wazawa. Hakika hili ni jambo la
kijasiri kwani mmesaidia kupunguza mzigo wa gharama kwa Serikali na kwa
Wananchi ambao walilazimika kufuata huduma hii nje ya nchi’.
Hata
hivyo amesema uwepo wa Kitengo cha Patholojia ni faraja pia katika
kuharakisha matibabu kwani hapo awali ilibidi sampuli zipelekwe Dar es
Salaam ili kubaini kama ni saratani au la. Utaratibu huu ulikuwa
unachelewesha kupata kwa zaidi ya wiki moja hadi mbili.
"Sampuli
inatolewa na majibu yanatoka ndani ya kipindi kifupi na wanaobainika
kuwa na saratani wanaanzishiwa tiba mapema. Vitengo hivi viwili lazima
vifanye kazi kwa karibu kwani vinategemeana sana".
Naye
Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Aliphonce Chandika
amesema takwimu za shirika la IARC chini ya WHO zinaonyesha kwamba mwaka
2018 jumla ya watu 18.1 waligundulika kuwa na aina mbalimbali za
saratani duniani,kati yao watu milioni 9.6 walifariki kutokana na
magonjwa ya saratani.
Dkt.
Chandika amesema kuanzishwa kwa daftari maalum la kuratibu maradhi ya
saratani kanda ya kati mwaka 2018,saratani ya malango wa kizazi ndio
inaongoza kwa saratani zote zilizoratibiwa ikiwa na jumla ya wagonjwa
778 sawa na asilimia 32 ya saratani zote na asilimia 50 kwa saratani za
wanawake huku saratani ya tezi dume ikiongoza kwa wanaume ambapo
wagonjwa 265 waliratibiwa sawa na asilimia 39 kwa upande wa wanaume.
Dkt.
Chandika ameongeza kuwa umri unaoathirika zaidi na maradhi hayo ni kati
ya miaka 50 hasi 69 ambapo jumla ya wagonjwa 1089 sawa na asilimia 42.2
ya wagonjwa wote.
Serikali
ilijenga Hospitali ya Benjamin Mkapa, yenye uwezo wa kutoa huduma
bobezi na za kisasa kwa kiwango cha kimataifa katika magonjwa ya Figo,
Moyo na Matibabu ya Saratani, ili kuwezesha upatikanaji wa huduma hizo
hapa nchini na hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopewa rufaa kwenda
kupata matibabu haya nchi za nje kama India na Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment