HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 18, 2021

Benki ya CRDB yatangaza Ufadhili wa Masomo wa Sh. Milioni 50 kwa Wachezaji 26 wa Mashindano ya Taifa Ya Mpira Wa kikapu. “CRDB Bank Taifa CUP"


 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Abdallah Ulega, akizungumza katika hafla fupi ya kutangaza ufadhili wa masomo kwa wachezaji wa mashindano ya Taifa ya mpira wa kikapu “CRDB Bank Taifa Cup” iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Martin Warioba.
 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Abdallah Ulega (wa pili kulia), akimkabidhi, Abdul-aziz Abdulla  (katikati) kutoka Arusha cheti cha udhamini wa masomo ‘Scholarship’ uliotolewa kwa vijana waliofanya vizuri katika mashindano ya ligi ya taifa ya mpira wa kikapu CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile, Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Martin Warioba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Phares Magesa. Benki ya CRDB imetoa udhamini wa masomo kwa vijana 26 wenye jumla ya shilingi milioni 50.

 

 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Abdallah Ulega (wa pili kulia), akimkabidhi Nuru Mbaraka (katikati) kutoka Arusha cheti cha udhamini wa masomo ‘Scholarship’ uliotolewa kwa vijana waliofanya vizuri katika mashindano ya ligi ya taifa ya mpira wa kikapu CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile, Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Martin Warioba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Phares Magesa. Benki ya CRDB imetoa udhamini wa masomo kwa vijana 26 wenye jumla ya shilingi milioni 50.


  Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Abdallah Ulega, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliopata ufadhili wa masomo ‘Scholarship’ kupitia mashindano ya mpira wa kikapu ya CRDB Bank Taifa Cup yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana. Benki ya CRDB imetoa udhamini wa masomo kwa vijana 26 wenye jumla ya shilingi milioni 50.

 

 

Na Mwandishi Wetu

 

 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Abdallah Ulega ameipongeza benki ya CRDB kwa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Benki hiyo katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuleta hamasa kwa vijana katika michezo .

Naibu Waziri huyo ametoa pongezi hizo katika hafla fupi ya kutangaza ufadhili wa masomo kwa wachezaji wa mashindano ya Taifa ya mpira wa kikapu “CRDB Bank Taifa Cup” iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) na wadau wengine  ikiwamo Azam TV, Sanlam Insurance, Mayfair Insurance na Cool Blue.

Naibu Waziri Abdallah amesema pamoja na Serikali na wadau binafsi kuweka juhudi kubwa katika kuboresha sekta ya michezo nchini  lakini ipo haja ya kuweka mikakati endelevu ya kukuza vipaji vya mpira wa kikapu kuanzia ngazi ya chini.

“Nitoe rai kwa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kuweka mikakati endelevu ya kukuza vipaji vya mpira wa kikapu kuanzia ngazi ya chini. Tutumie shule zetu kufundisha mchezo huu mashuleni. Lakini pia tuanzishe na kuziendeleza shule za mchezo wa mpira wa kikapu (basketball academy). Sisi kama Wizara tumejipanga kikamilifu kushirikiana nanyi ilikuweza kufikia lengo”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Bi. Tully Mwambapa alisema udhamini huo wa masomo kwa wachezaji ni muendelezo wa jitihada za Benki ya CRDB katika kuwawezesha vijana wa Kitanzania kupitia michezo. Aliongezea kuwa Benki hiyo kupitia sera yake ya Uwezeshaji katika Jamii (CSI Policy) imekuwa ikiwekeza katika michezo ya vijana kwa kuamini kuwa inasidia kuongeza ushiriki wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii.

 

“Kwa kutambua haya Benki ya CRDB kupitia sera yake ya uwekezaji katika jamii “Corporate Social Investment Policy” iliona ni vyema kuambatanisha suala la elimu na michezo na hivyo kutangaza ufadhili wa masomo kwa vijana ambao wameonyesha uwezo mkubwa katika mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup. Hii ilikua ni mbali ya zawadi zilizotoloewa kwa timu zilizofanya vyema pamoja na wachezaji binafsi”.

Akizungumzia kuhusu msukumo uliopelekea Benki hiyo kudhamini masomo ya wachezaji wa mpira wa kikapu Tully alisema mchezo wa mpira wa kikapu umekuwa haupewi sana kipaumbele kulinganisha na michezo mingine, Hivyo kupelekea kuwakatisha tamaa vijana wengi ambao wamekuwa wakionyesha vipaji katika mchezo huo.

“Baada ya mchakato mrefu wa kufanya tathimini ya uwezo uliooneshwa na vijana pamoja na kufatilia taarifa zao za kielimu, tumefanikiwa kukamilisha zoezi hilo na leo tupo hapa kwa ajili ya kutangaza vijana waliofanikiwa kupata nafasi hizo za ufadhili wa masomo kwa mwaka 2020/2021”. Alisema Tully.

Kwaupande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Phares Magesa ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwekeza katika mpira wa kikapu huku akisema udhamini huo wa masomo utakwenda kuleta hamasa zaidi kwa vijana wengi kushiriki katika mchezo huo.

Hafla hiyo ya kutangaza udhamini wa masomo kwa vijana hao ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa mchezo wa kikapu ikiwamo Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB na mchezaji wa zamani wa timu ya mpira wa kikapu ya Pazz, Martin Warioba, Afisa Uendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwile, Mkurugenzi Mkuu wa Sanlam Insurance, Khamis Suleiman, Msimamizi wa Vipindi vya Michezo Azam TV na wawakilishi wa Mayfair Insurance na Cool Blue ambao wote walikuwa wadhamini wa mashindano hayo.

Mashindano ya CRDB Bank Taifa Cup yakiwa yamebeba kauli mbiu ya “Ni Zaidi ya Game, Ni Maisha” yalizinduliwa tarehe 7 mwezi wa kumi mwaka jana na kufanyika kwa mafanikio makubwa jijini Dodoma katika viwanja vya Chinangali kuanzia tarehe 12 hadi 21 mwezi Novemba mwaka jana ambapo timu 36 za mpira wa kikapu kwa upande wa wanaume na wanawake zilichuana.

No comments:

Post a Comment

Pages