HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 19, 2021

KAGERA YAJIVUNIA MAFANIKIO SEKTA YA ELIMU

 

Rais John Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti.

 

 Na Lydia Lugakila, Bukoba

Mkoa wa Kagera umefanikiwa katika sekta ya elimu kwa kupungua kwa utoro kwa asilia 3 huku ongezeko la wanafunzi ikiwa ni asilimia 16 na 30 Kati ya shule za awali msingi na sekondari.

Akielezea mafanikio hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa mkoa huo umefanikiwa katika sekta ya elimu tofauti na miaka ya nyuma ambapo kwa sasa wamefanikiwa kuthibiti utoro kwa asilimia 3.

Brigedia Jenerali Gaguti amesema kuwa shule za msingi ufaulu umeongezeka kwa asilimia 88.8 na shule za sekondari ni asilimia 90.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amempongeza Rais Magufuli kwa miradi mbalimbali ya kimaendeleo aliyoitekeleza katika mkoa huo ukiwa ni pamoja na uwekezaji, maji, miundombinu ya barabara usafiri na usafirishaji.

Akizungumza suala la uwepo wa hifadhi ikiwemo hifadhi ya Burigi Chato eneo la msitu wa Biharamulo mkuu huyo wa mkoa amemshukuru Rais Magufuli kwa kuimarisha ulinzi na usalama kwani eneo la msitu huo lilikuwa korofi kiusalama ambapo Kati ya mwaka 2010 - 2015 matukio ya kiuharifu yapatayo 124 ya kutumia siraha yamepungua yapata miaka miwili sasa.

Rais wa Magufuli yupo ziarani mkoani Kagera kwa shughuli ya uwekaji mawe ya msingi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages