HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 07, 2021

KALANGUTI AWEKA MIKAKATI MADHUBUTI YA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KWA WANANCHI WAKE


Diwani wa Kata ya Tangini Mfalme Kalanguti akizungumza jambo na baadhi ya wananchi ambao pia ni wafanyabiashara wadodowadogo kuhusiana na mipango yake aliyojiwekea katika suala zima la kuwaletea maendeleo pamoja na kuboresha mazingira ya usafi ili kuondokana na chanagmoto ya magonjwa ya milipuko. (PICHA NA VICTOR MASANGU).

 

 

NA  VICTOR MASANGU, KIBAHA 

 

Diwani wa Kata ya Tangini iliyopo katika Halmashauri ya Kibaha mji kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Mfalme Kabuka amewaasa wafanyabiashara kuhakikisha kwamba wanazingatia

Akizungumza na baadhi ya wafanyabishara wadogo wadogo wanaofanya shughuli zao katika soko la Mnalani  kuhusiana na mikakati yake aliyojiwekea  baada ya kuchaguliwa  katika  kuimarisha hali ya usafi wa mazingira kwa lengo la kuweza kuwa na  afya njema kwa wananchi na kuondokana na magonjwa mbali mbali ya mlipuko.

 

“Mimi Kama Diwani wa Kata hii ya Tangini lengo langu kubwa ni kuweka mipango ambayo itaweza kuwasaidia wafanyabiashara wadogowadogo katika soko hili la mnalani ,hivyo nitashirikiana bega kwa bega na viongozi wenzangu wa halmashauri ili kuweza kuwapa fursa wafanyabiashara kufanya kazi zao bila ya kupata magonjwa yoyote ya mlipuko kama vile kipindupindu, na magonjwa mengine ambayo yanasababisha na uchafu wa mazingira.

Aidha alibainishwa kwamba katika kuunga juhudi za agizo la Makamu wa Rais Mama Sami Suluhu la kufanya usafi wa mazingira katika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi amedai kwa upande wake atawashirikisha wananchi wake ili kuhakikisha kwamba wananeo yote yanakuwa katika hali ya usafi kwa kufanya usafi huo kwa kila mwisho wa juma la wiki.

“Katika Soko letu la Mnalani bado kuna baadhi ya changamoto ambazo zinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu kama vile kuweka mikakati ya miundombinu mizuri ya maji ili mvua inapoanza kunyesha maji yasiweze kukwama na pia kuweka sehemu maalumu kwa ajili ya shimo la kutupiatakakata hii itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuondokana na magonjwa ya mlipuko,”alisema Kabuga.

Katika hatua nyingine Diwani huyo alitoa wito kwa wafanyabiashara wote kuachana kabisa na tabia ya kutupa takataka ovyo na badala yake wahakikishe wanaweka utaratibu za kuziweka sehemu moja ili ziweze kuchukiliwa kwa utaratibu uliopangwa na kwenda kuzichoma katika sehemu ambayo imepangwa maalumu.

Pia aliongeza kuwa katika kukabiliana na wimbi la magonjwa mbali mbali ya mlipuko wananchi wote wanapashwa kuendesha shugghuli zao kwa kuzingatia sheria za na taratibu ambazo zimewekwa na kuheshimi miongozo yote ambayo inatlewa na wataalamu wa afya lengo ikiwa ni kuweza mazingira yawe katika hali ya usafi.

Pia Diwani huyo alimpongeza Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli kwa juhudi zake ka kuboresha sekta ya afya pamoja na kupambana vilivyo na kufanikiwa kumalizika kabisa kwa ugonjwa wa Covid 19 ambapo aliweza kufanya juhudi za makusudi hadi kufikia hatua ya kuumaliza kabisa katika maeno mbali mbali.

No comments:

Post a Comment

Pages