Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzana Raymond wakati wa kuzindua mfumo wa Takukuru ambayo inatembea kwa wananchi wa kijiji cha Kwala kilichopo katika halmashauri ya Kibaha vijijini Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kutoa elimu kuhusiana na masuala mabali mbali ya rushwa. (Picha na Victor Masangu).
VICTOR MASANGU, KIBAHA
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani katika kukabiliana na wimbi la kupokea na kutoa rushwa limekuja na programu maalumu ambayo itakuwa na lengo la kuweza kusikiliza kero , kesi na malalamiko mbali mbali ambayo yanakuwa yanatolewa na wananchi ili yaweze kufanyiwa kazi kwa haraka zaidi na kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Suzana Raymond wakati wa kuzindua mfumo wa Takukuru ambayo inatembea kwa wananchi wa kijiji cha Kwala kilichopo katika halmashauri ya Kibaha vijijini Mkoa wa pwani kwa ajili ya kutoa elimu juu ya masuala ya rushwa pamoja na kutoa fursa za kusikiliza kero za wananchi hao ambao wamekuwa wakipata shida ya kufika katika ofisi husika.
“Katika kuhakikisha kwamba sisi kama Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru Mkoa wa Pwani tuanwafikia wateja wetu wakubwa ambao ni wananachi tumeanzia mpango huu wa Takukuru ambayo inatembea katika maeneo mbali mbali kwa lengo la kuwafikia kwa urahisi wananachi mabo wanakabiliwa na changamoto mbali mbali na kwamba kwa sasa tumeanzia kwa wananchi wa Kwala.”alifafanua Suzana.
Pia akizungumza katika uzinduzi huo ambao uliohudhuliwa na wananchi kutoka vijijini mbali mbali vilivyopo katika kata ya Kwala pamoja na maafisa wa Takukuru Mkuu huyo alisema, kwamba mfumo wa taasisi ya Takukuru ambayo inatembea itakuwa inawafikia wananchi katika maeneo mbali mbali kulingana na ratiba ambayo imepangwa ya ya kila Alhamisi ya mwisho wa mwezi.
Suzana alisema kwamba kuanzishwa kwa TAKUKURU inayotembea itawapa fursa wananchi ambao wanashindwa kufika ofisi za Taasisi hiyo kutokana na umbali au matatizo mengine ambayo ni kiwazo kufikisha kero zao kwa wahusika zitafutiwe ufumbuzi.
Suzana alisema kwa utaratibu huo kero zitafatuliwa kwa haraka na kwa zile zinazohitaji ufuatiliaji zitachukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi na baadae wahusika watapewa mrejesho.
" TAKUKURU inayotembea itakuwa inasikiliza kero za wananchi, zinazowezekana vinatatuliwa papo hapo na nyingine tunazichukua kwenda kuzifanyia kazi " alisema Suzana.
Katika mkutano huo wananchi waliibua suala la malipo ya fidia ya maeneo yao ambayo yamepitiwa na reli ya mwendokasi, pamoja na migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo kwa kiasi kikubwa inapelekea kukwamisha shughuli mbali mbali za uzalishaji pamoja na kilimo.
Suzana alifafanua kuwa ofisi yake ya Takukuru imechukua kero hizo mbali mbali ambazo zimetolewa na baaadhi ya wananchi na kwamba ameahidi kuzifanyia kazi i, ambapo katika suala la mambo ya fidia za wananchi aliahidi kufanya mawasiliano na mamlaka husika ya TRC na kuhusiana na migogoro ataanzia kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Martine Ntemo ili kuweza kuwasaidai wananchi kuondokana na kero hizo..
No comments:
Post a Comment