HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 05, 2021

VIJANA WA KITANZANIA WAFUNDWA


Mwinjilisti wa kanisa la Angalikana Dayosisi ya Centrel Tanganyika Dodoma Festo Machella akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kuwahmiza vijana kufanya kazi kwa bidii ili kujiinua kiuchumi.  
 

 

NA DANSON KAIJAGE, DODOMA


IKIWA ni siku nne tangu kuanza kwa mwaka.2021 vijana wametakiwa kubadilika na kubuni miradi mbalimbali ya kuwaingizia kipato badala ya kukaa vijiweni na kulalamika kuwa uchumi ni mgumu.


Kauli hiyo imetolewa na mwinjilisi wa kanisa Kuu la Anglikana Festo Machela alipokuwa akizungumza na vijana juu ya kubadilisha mwelekeo wa maisha badala ya kuendelea na mazoea.


Mwinjilisti huyo amesema kuwa vijana ni nguvukazi kubwa katika taifa na hakuna kijana ambaye anaweza kupata fedha za bure badala yake wanatakiwa kubadilisha mwelekeo wa kubuni miradi ambayo inaweza kuwaingizia kipato kwa faida yao wenyenye na taifa kwa ujumla.


Akizungumza na vijana hao leo katika eneo la Nzuguni amesema pamoja na kuwa mwaka 2020 ulikuwa mwaka wenye changamoto mbalimbali lakini mwaka huu ni mwaka ambao iwapo watu watapambana watapata mafanikio.


"Pamoja na mambo mengini ni wajibu wa kila kijana wa kitanzania kuhakikisha anajipanga kufanya kazi kwa bidii kubwa kwa ubunifu badala ya kukaa vijiweni na kubishania juu ya timu za mpira.


" Ni wakati wa kufanya kazi kweli kweli na kwa bidii kubwa hakuna sababu ya kufanya kazi kwa ulegevu maana hata maandiko nanasema apandaye baba atavuna baba apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu"amesema Machela.


Kiongozi huyo amesema kuwa taifa haliwezi kufikia uchumi wa kati au uchumi wa viwanda kama vijana wake watakuwa wavivu,ombaomba au watu wa kutegemea zaidi misaada.


Kutokana na hali hiyo amewataka hata vijana wanaomaliza elimu ya juu kuwa chachu ya maendeleo kwa kubuni miradi yenye tija kwao badala ya kusubili ajila toka serikalini.


Akizungumzia masuala ya Kiroho Machella amewataka watanzania kuhakikisha wanamcha Mungu na kufanya kazi zao kwa uadilifu zaidi.


"Ili kuwa na taifa lenye viongozi waadilifu wenye uchungu na wanaowaongoza ni lazima wawe viongozi wenye hofu ya Kimungu.


" Uwezi kuwa na taifa bora kama siyo wacha Mungu, nankama viongozi watakuwa wacha Mungu na kujawa hofu ya Kimungu ni wazi kuwa vitendo vya uonevu,ulaji wa Rushwa,Ufisadi na unyanyasaji havitakuwepo"amesema Machella.


Aidha amewataka viongozi wa dini kutimiza wajibu wao kwa kuwaubiria watu ukweli na kutangaza neno la Mungu kwa bidii bila kujali cheo au nafasi ya mtu aliyonayo.


"Kazi ya mtumishi wa Mungu ni kuhakikisha anasema ukweli ili kuwaponya anaowaongoza na kuliponya taifa kwa ujumla wake.


" Vivyo hivyo watumishi wa serikali pamoja watumishi wa Umma kila mmoja atimize wajibu wake kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi bila kumuonea mtu wala kumnyanyasa"amesisitiza Mwinjilisti Machella.

No comments:

Post a Comment

Pages