HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 05, 2021

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, ATEMBELEA OFISI ZA BODI YA MIKOPO

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga akisalimiana na Mkurugenzi wa Uchambuzi na Upangaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Dkt. Veronica Nyahende wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuitembelea Ofisi ya HESLB, Tazara Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na menejimenti ya HESLB Jumatatu (Januari 4, 2020).

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru (kulia) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga (kushoto) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuitembelea Ofisi ya HESLB, Tazara Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na menejimenti ya HESLB. Katikati ni Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo wa HESLB, George Mziray.

 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga akipokea moja ya machapisho yanayochapishwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakati wa ziara ya kikazi ya kuitembelea Ofisi ya HESLB, Tazara Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na menejimenti ya HESLB.

 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuitembelea Ofisiya HESLB,Tazara Jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na menejimenti ya HESLB. (PICHA NA BODI YA MIKOPO-HESLB).

No comments:

Post a Comment

Pages