HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 06, 2021

WANASIASA WAONGEZEWA MAARIFA


Diwani wa Viti Maalum Hilda Kadunda (CCM) akiwa katika duka lake la kuuza asali mbichi kama sehemu ya ujasiriamali.

  

NA DANSON KAIJAGE, DODOMA 

WANASIASA wamekatika kuwa kielelezo sahihi kwa wanaowaongoza kwa kufanya shughuli za maendelea hasa katika uzalishaji mali.


Kauli rai hiyo imetolewa na diwani wa viti Maalum Hilda Kadunda (CCM) wilaya ya chamwino tarafa Makanghwa mkoani Dodoma.


Akizunguzia mwelekeo wa kiuchumi 2021 Hilida amesema kuwa ili kuwa na maendeleo kwa jamii ni vyema viongozi wa kisiasa wakaona uwezekano wa kufanya mambo ya kijamii,kisiasa pamoja na mambo yao binafsi ya kujiingizia kipato ili kuwa mfano kwa wale wanaowaongoza.


Mwanasiasa huyo amesema wanasiasa wanatakiwa kutenga muda wao vizuri kwa lengo la kuihudumia jamii huku wakiwekeza badala ya kusubiria posho za vikao au mishahara kulingana nannafasi zao za kazi.


Amesema ili kupata taifa lenye maendeleo ni muhimu kufanya uwekezaji ikiwa ni biashara,kilimo au ufugani na kueleza kuwa iwapo watafanya kwa kufuata misingi bora na sheria za nchi itakuwa chanzo cha wananchi nao kuvutiwa na kuiga kinachofanywa na wanasiasa.


Diwani huyo ambaye kwa sasa anaeleza kuwa amewekeza katika kilimo,ujasiliamali amesema amelazimika kufanya hivyo ili anapokuwa akiwaeleza wananchi kujishughulisha kiuchumi awe na ujasili kutokana nankile ambacho anakifanya na kinaonekana.


"Mimi ni Diwani wa Viti maalumu hiki ni kipindi changu cha pili lakini lazima kujua kuwa diwani siyo kufanya kazi ya siasa tu,lazima kutenga muda wa kuwahudumia wananchi pamoja na kufanya shughuli za kiuchumi.


" Tumekiwa tukimsikia Rais wetu Dk.John Pombe Magufuli  akihimiza uwekezaji,uchapaji wa kazi kwa maana hiyo siyo sahihi kwa mwanasiasa kuzunguka tu kufanya siasa bila kuonesha mfano wa yeye anafanya nini.


"Kama kilimo mwanasiasa anatakiwa kulima tena kilimo cha kisasa hata unapokuwa ukizungumza na wananchi juu ya kulima kilimo cha kisasa unaweza kuwatolea mfano kwa shamba lako na wananchi wakavutiwa na kujikuta wanafanya vizuri zaidi.


" Tusipofanya hivyo hakika nataka kukuambia kuwa itakuwa kazi bure ni sawa kupiga kelele ya kuzuia upokeaji nanutoaji wa rushwa wakati wewe ni kinara wa kipokea au kutoa"amesema Diwani Kadunda.


Akizungumzia suala la utunzaji wa mazingira Diwani huyo ameihamasisha jamii ya wanachi Loje kuhakikisha wanapanda miti ya kivuli na matunda kwa ajili ya kuweka mazingira sawa.


"Kwa sasa ni kipindi cha msimu wa mvua ni vyema ikapandwa miti ya kivuli na matunda sambamba na kupanda mazao ambayo yanaendana nanhali ya hewa na yanayoweza kuvunwa kwa muda mfupi" amehimiza diwani Kadunda.

No comments:

Post a Comment

Pages