HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 19, 2021

Watu Milioni 100 mpaka150 utumia kiswahil


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo Januari 19, 2021. (Picha na VPO).


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua Vitabu vya Mkakati na Muongozo wa kufundishia Lugha ya Kiswahili kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili yaliyoadhimishwa leo Januari 19, 2021 katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi, Wajumbe, Wadhamini na Wafanyakazi wa  Taasisi za Kiswahili baada ya Kufungua Maadhimisho ya Siku ya kiswahili katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma leo Januari 19, 2021.

 

 

Na Hamida Ramadhan, Dodoma


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 100 mpaka 150 utumia Lugha ya kiswahili kwa ajili ya mawasiliano  na kuzitaka taasisi binafsi kuendeleza kutumia lugha hiyo.

Aliyasema hayo jana Jijini Dodoma wakati  alipokuwa kwenye Maadhimisho ya siku ya kiswahili Kitaifa yaliyoandaliwa na mabaraza ya Tanzania bara (BAKITA) na Tanzania Zanzibar (BAKIZA)huku kauli mbiu ikisema"Bidhalisha Kiswahili kwa maendeleo endelevu ya Tanzania".

Aidha alisema kuwa lugha ya kiswahili imekuwa na matumizi mapana huku ikitumika ndani na nje ya nchi kwa kufundishia kwenye vyuo vikuu vya kimataifa  mbalimbali pamoja na shule za sekondari na msingi .

Alisema kuwa lugha ya kiswahili imekuwa ikisikika kwenye Radio za kimataifa ikiwemo BBC na Radio Amerika huku kiswahili kikitumika kama bidhaaa ya kukuza kiuchumi.

Hata hivyo alisema katika kukuza kiswahili, Awamu hii ya tano kupitia Rais John Magufuli  ameweza kukiwekea mkazo kukitumia kwenye mikutano mbalimbali na hata kukitumia nje ya nchi wawapo kwenye mikutano.

"Hapo awali hakukuwa na msisitizo kwenye mikutano kuongea kiswahili lakini kupitia Rais wetu John Magufuli ameweza kuimarisha ambapo mikutano inaendeshwa kwa lugha ya kiswahili na sio kiingereza kama mwanzoni  "alisema 


"Nawaomba Taasisi binafsi wasikionee haya Kiswahili kukitumia katika ofisi zao,kwani hiyo ni.mojawapo ya kuendeleza matumizi ya lugha yetu ya Kiswahili kwani Taasisi binafsi asilimia kubwa wanaofanya kazi ni Watanzania amabo wanaongea lugha ya Kiswahili,hivyo wasione ubaya kukitumia lugha ya mawasiliano hivyo Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA na lile la  Zanzibar BAKIZA kuongeza wigo wa misamiati inayoeleweka"alisema

Makamu huyo wa Rais alitolea mfano neno kusimikwa ambalo alisema kwa upande wa Zanzibar ni neno Kali lenye maana tofauti limitamkwa huku Tanzania Baram.

" Nimekuwa nikiingiwa na ukakasi katika kutamka neno la kusimikwa kwa maaskofu, kwani neno Hilo kwetu Zanzibar si neno la kutamkwa hadharani", alisema Suluhu.

Aidha Makamu wa Rais alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuendeleza Kiswahili kwa kuandaa kamusi yenye maneno Millioni 50, lakini mpaka Sasa umefikia maneno Millioni 1.5.

Suluhu pia aliwataka Wakurugenzi wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo kutoa fungu kwa kuendeleza lugha ya Kiswahili kwa kuangalia maeneo ambayo Kiswahili hakitumiwi Sana.

Alisema kuwa BAKITA na BAKIZA wapewe Rasimali Watu,Fedha na watalaamu na kutoa machapisho yachapishwe kwa wingi ili yasambazwe sehemu mbalimbali.

Naye Naibu Waziri wa Habari Utamaduni.na Michezo Abdallah Ulega alisema Lugha ya Kiswahili inaenea kwa Kasi, kwani Leo lugha hiyo imekuwa si Mali ya pekee imekuwa ikitumiwa nchi nyingi Duniani.

" Hivi Sasa Duniani Kiswahili no bidhaa ambayo, Watangazaji,waandishi wa habari, watafsiri Wana soko kubwa la kupata kazi"' alisema Ulega.

Katika maadhimisho hayo Makamu wa Rais alizindua kitabu chenye muongozo wa kufundishia watu kutoka nje .


No comments:

Post a Comment

Pages